Je, Tanzania ianze kukata hela ya kutunza watoto wa nje ya ndoa kwenye mshahara wa mwanaume?

Sep 27, 2015
17
45
Kama tunavyofahamu kuna wanaume wengi hukimbia majukumu yanayoendana na kuitwa baba huku mtaani akijisifu yeye ni kidume na kumuachia mwanamke mzigo wote wa matunzo ya mtoto.

Je, kuwakata hela ya matunzo ya mtoto moja kwa moja kutoka kwenye mshahara itapunguza wimbi la wanaume wanaowalaghai kisha kuwatelekeza wanawake baada ya kupata mimba zao?
 

Tyta

JF-Expert Member
May 21, 2011
12,799
2,000
asilimia kubwa ya wananchi wake hawako kwenye mifumo rasmi utaanzaje kuwakata?.....
 
Sep 27, 2015
17
45
Kwa wale waliopo wakatwe hivyo lakini kwa wale walio nje basi iwe kama marejesho ya mkopo wa bank ikisimamiwa kwa umakini na ustawi wa jamii
 

BISECKO

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
538
1,000
Kama tunavyo fahamu kuna wanaume wengi hukimbia majukumu yanayo endana na kuitwa baba huku mtaani akijisifu yeye ni kidume na kumuachia mwanamke mzigo wote wa matunzo ya mtoto.je kuwakata hela ya matunzo ya mtoto moja kwa moja kutoka kwenye mshahara itapunguza wimbi la wanaume wanao walaghai kisha kuwatelekeza wanawake baada ya kupata mimba zao??
Sheria iko wazi katika kulinda maslahi ya mtoto na mama kuhusiana na suala la malezi ili kuhakikisha mama haelemewi na mzigo na hii ni kama ifutavyo:

1. Ni wajibu wa kisheria wa baba au mwanaume kuhusika katika matunzo ya mtoto wake ama aliye kwenye malezi yake ama malezi ya mtu mwingine, hii ni kwa kumpatia mahitaji Kama vile chakula, mavazi na elimu vile ipasavyo kwa kuzingatia kipato chake (anaweza fanya hivyo kwa kulipa gharama).


2. Mahakama yaweza toa amri wakati wowote kwa mwanaume kulipa gharama za matunzo kwa manufaa ya mtoto wake katika mazingira kadhawa km vile:

i) Endapo amekataa au amepuuzia kutoa matunzo ya kutosha.

ii)Endapo amemtelekeza mke wake na mtoto wakiwa chini yake n.k. Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya ndoa ya 1977.
 

vanmedy

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
2,451
2,000
Kama tunavyo fahamu kuna wanaume wengi hukimbia majukumu yanayo endana na kuitwa baba huku mtaani akijisifu yeye ni kidume na kumuachia mwanamke mzigo wote wa matunzo ya mtoto.je kuwakata hela ya matunzo ya mtoto moja kwa moja kutoka kwenye mshahara itapunguza wimbi la wanaume wanao walaghai kisha kuwatelekeza wanawake baada ya kupata mimba zao??
Ili tuzidi kutegesheana mimba bila mahesabu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom