Je, Tanzania haiwezi kupiga marufuku uingizwaji wa nguo za mtumba, Yapi madhara?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,106
2,000
Baadhi ya nchi ikiwemo Rwanda walishapiga marufuku nguo za mkono wa pili.

Je, Tanzania hatuwezi kuiga mfano huu wa kuvaa nguo kuu kuu walizovaa mabeberu huku nyingine wakitapikia na kukojolea.

Je, tufanyeje? What is the economic implication kama tukiamua.

Wadau leteni mawazo tupate suluhisho. Je ni kwamba Hatuna viwanda.

Je, ni kwamba nguo tunazozalisha ndani hazitoshi?
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
25,401
2,000
Nyerere alifanya hilo jambo Miaka ya mwisho ya 70 mpaka ya mwanzo ya 80

Ilikuwa jambo la kawaida kukuta Mwanaume Mtu mzima kavaa midabwada ya Urafiki Na Sungura Tex barabarani iliyochakaa Na kuwekwa Viraka Kwenye Makalio

Tengenezeni nguo nzuri kwa bei reasonable Hii mitumba yenyewe itapotea kwa kukosa Soko

Mnataka nguo ziadimike Kama Sukari?
 

h120

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
2,420
2,000
Niliona habari moja ITV wananchi wa Rwanda wakilalamikia bei ghali ya nguo zinazotengezwa huko kwao na ubora hafifu, nadhani ni jambo zuri ila yahitaji kujipanga kwa viwanda vya ndani.
 

Masamila

JF-Expert Member
Jun 22, 2014
6,154
2,000
Tatizo ni umasikini ndugu na sio aina ya nguo. Kuna watu sandals tu zinawashinda vipi mkalazimisha nguo mpya?
 

Nukta5

JF-Expert Member
Jun 7, 2014
1,139
2,000
Uzeni ndege zote, nunua mitambo mipya, wekezeni hela kwenye zao la pamba, leteni wawekezaji toka china wakae Urafiki, Mwatex, Motex madisigner wapo wakutosha hata kama hakuna waziri anaenda kiwandani na sample za nguo za mtumba anawaambia nataka quality za nguo ziwe namna hii kwa gharama hii.
China wangefunga viwanda vyote vya nguo, ingebidi tutanue viwanja vyetu vya ndege kwa exportation.
Pesa nyingi sana tunapoteza kwa kuruhusu watu kwenda china kuleta nguo ambazo hazina quality. Wa dada wa mjini alishafanikiwa kupata kitako basi anafanya biashara ya nguo kila mdada mjini anaenda china kuleta nguo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom