Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,480
- 5,506
Kama ilivyo ada na kwa jinsi hali ya hewa ya siasa ilivyo kwa sasa ni wazi kabisa kwamba sasa ni Rasmi JPM ndiye mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM. Tunatambua kuwa JPM anayo nia, sababu na uwezo wa kuhakikisha kwamba anabaki madarakani katika kipindi kingine cha miaka mitano.
Mengi yamejitokeza katika kipindi cha miaka mitano iliopita ambayo kwa hakika yanatufanya Watanzania tujiulize tunataka Rais wa namna gani?
Kabla ya Magufuli kila mtu alitaka Rais kama Magufuli,kwa hakika tulitaka Rais ambaye ni mara mbili au tatu ya Magufuli,wengi walitaka Rais mwenye msimamo thabiti,mkali na anayesimamia haki na uwajibikaji. Kwa kiasi ametenda kwa kuzingatia matarajio hayo ingawa sio kwa kiwango tulichotarajia hakukaza ipasavyo,hakuwa na msimamo ipasavyo kuna maeneo ambayo bado alilega lega.
Kwa kuzingatia hatua iliyofikia katika maendeleo ya taifa letu na kwa kuzingatia changamoto tulizo nazo kama taifa na aina ya mabadiliko tunayotaka je Tanzania bado inahitaji Rais mwenye sifa kama za Magufuli?Kama jibu ni hapana je tunahitaji Rais mwenye sifa gani?Uwezo gani na haiba gani?
Ni maeneo gani ambayo tunahitaji mabadiliko ya kiongozi?Je, ni katika uhuru wa vyombo vya habari?Je ni katika siasa?Je, ni katika sera za uchumi, je ni katika huduma za kijamii?Je, ni katika miundo mbinu?Je, ni katika mahusiano ya kimataifa?Je, ni mabadiliko ya aina gani tunayotaka?Je, tunafikiri tunahitaji kiongozi mwenye sifa gani?
Tutoe maoni kwa uwazi kwa kuzingatia changamoto zilizopo,huku tukiwa na imani kwamba kiongozi atakayechaguliwa atazingatia hayo
Karibuni kwa mjadal