Je, tangu mwaka 1987 hadi sasa kuna mwana jf amewahi kusikia hili?

Papa D

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
753
182
Viongozi wengi walopata mafanikio katika uongozi wao sehemu mbalimbali Duniani hawakuacha kusema maneno haya kwenye hotuba zao:- "......for the future Generation/...... kwa vizazi vijavyo"

Nimefuatilia viongozi wa TZ wenye ngazi ya kuanzia ukuu wa mkoa hadi Rais. Kinogozi wa mwisho kusema maneno hayo katika hotuba zake ni Mzee mwinyi mwaka 1987 [ off course with the exclusion of Nyerere].
Wana JF kwa nini viongozi wetu wanaogopa/wanashindwa kutuonyesha hisia zao kwa vizazi vijavyo?
 
Mkuu raisi Kikwete kaingia madarakani 2005 kwa kunadiwa kama "raisi kijana". December Pinda kaenda kutembelea kituo cha kulelea watoto yatima na aka sema kwenye moja ya sentensi zake kwamba yeye ni "kijana anaelekea uzeeni". Sasa una tegemea hawa viongozi wanao jiona forever young wata fikiria kizazi kijacho? Wakati kwa mawazo yao wao bado ndiyo the next generation...
 
Hawaa hawapo kutengeneza future ya mtu isipokuwa ya kwao, wake zao, ndugu zao na watoto wao. Hivyo, hawana sababu ya kuzungumzia future ya mtu.
 
Wote sio viongozi bali ni wanasiasa. Kawaida ya wanasiasa huzungumzia "NEXT ELECTION" hata siku moja hakuna "next generation".
 
Kama current generation inawatesa kiasi hiki, kweli watapata hata idea ya kuwaza kizazi kijacho?
 
Badala ya kusema "vizazi vya baadae", husema "Vijana ndio Taifa la kesho", sawa sawa na wenye maduka uchwara wanpoandika "MKOPO KESHO". Wanasiasa wetu kama wenye maduka uchwara husema hivi wakiamini kuwa "kesho haipo", ukienda kesho, rudi kesho.

Kwa mwanasiasa ambaye anaamini leo tu kwa maslahi yake, wala hajihangaishi kufikiria kesho Taifa hili litakuwa vipi. Ndio maana, kwa mfano, elimu yetu imefikia kiwango cha chini kabisa, mashirika ya umma yanaumwa, hawana ubunifu wala ugunduzi wa kulinasua taifa na umasikini. Ubunifu wao ni janja gani, mwanya gani watautumia "kuchota chao mapema, leo...kesho au "future" ya nini?
 
Mkuu raisi Kikwete kaingia madarakani 2005 kwa kunadiwa kama "raisi kijana". December Pinda kaenda kutembelea kituo cha kulelea watoto yatima na aka sema kwenye moja ya sentensi zake kwamba yeye ni "kijana anaelekea uzeeni". Sasa una tegemea hawa viongozi wanao jiona forever young wata fikiria kizazi kijacho? Wakati kwa mawazo yao wao bado ndiyo the next generation...

vema kamanda, kumbe umegundua vilaza wetu.
 
Tanzania tanzania, nakupenda kwa moyo wote, nchi yangu tanzania jina lako ni tamu sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom