Je, tafsiri nyingine ya sheria inayoongoza Bunge letu, ni ipi nje ya hii iliyotumika kumuadhibu Sophia Simba?

waco1920

Member
Oct 20, 2020
14
33
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuutarifu Umma kuwa; kwa mujibu wa Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa; kufuatia Mbunge wa Viti Maalum, SOPHIA MNYAMBI SIMBA kufukuzwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi tarehe 11 Machi, 2017 kiti cha Mbunge huyo wa Viti Maalum Wanawake kwa tiketi ya CCM kiko wazi.

Kwa mujibu wa Ibara ya 67 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ili mtu ateuliwe au achaguliwe katika nafasi ya Ubunge ni lazima awe mwanachama aliyependekezwa na Chama chake husika cha Siasa.

Kwa kuwa Ndg. SOPHIA MNYAMBI SIMBA amefukuzwa uanachama wa Chama kilichomdhamini, Ibara ya 67 (2) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaelekeza kuwa Mbunge huyo amepoteza sifa za kuteuliwa au kugombea Ubunge.

Kutokana na kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge wa Viti Maalum, taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Jaji (R) Semistocles Simon Kaijage Mwenyekiti TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI 12 Aprili, 2017 Maelezo haya ndiyo yanayotakiwa kwa hakina halima na hakuna hoja nyingine mbadala Wala siyo jukumu la spika kuwa sehemu ya mgogoro

Akijibu hilo swali wakati akizungumzia kauli ya Mzee Msekwa alisema wanahabari hebu waacheni wastaafu wapumzike huku nyuma mambo yalishabadilika sasa sijui huenda hata hatujui huenda katiba ilishabadilishwa unaweza kushangaa hicho kifungu cha katiba kilishafanyiwa amendment mkuu

Wee hukuona wala basi kusikia kwenye hbr ya kina Mwambe, Lijualikali, Silinde nk na nini kilitokea

Kwa hiyo usiing'ang'anie sana hiyo katiba mkuu kwa sasa
 
Tanzania hatuna katiba bali tunaongozwa na matakwa ya watu sio katiba, Katiba yetu ilianza kuvurugwa tangu Rais wa serikali ya ccm wa sasa alipoingia madarakani.
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuutarifu Umma kuwa; kwa mujibu wa Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa; kufuatia Mbunge wa Viti Maalum, SOPHIA MNYAMBI SIMBA kufukuzwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi tarehe 11 Machi, 2017 kiti cha Mbunge huyo wa Viti Maalum Wanawake kwa tiketi ya CCM kiko wazi.

Kwa mujibu wa Ibara ya 67 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ili mtu ateuliwe au achaguliwe katika nafasi ya Ubunge ni lazima awe mwanachama aliyependekezwa na Chama chake husika cha Siasa.

Kwa kuwa Ndg. SOPHIA MNYAMBI SIMBA amefukuzwa uanachama wa Chama kilichomdhamini, Ibara ya 67 (2) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaelekeza kuwa Mbunge huyo amepoteza sifa za kuteuliwa au kugombea Ubunge.

Kutokana na kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge wa Viti Maalum, taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.

Jaji (R) Semistocles Simon Kaijage

Mwenyekiti

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

12 Aprili, 2017

KUTOKA MAKTABA

Maoni yangu ni kwamba hii sheria ipo kwa ajili ya watu fulani.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom