Je, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa iliundwa ili kupunguza au kuondoa rushwa na ufisadi au iliundwa ili kuwahadaa mabeberu watusaidie zaidi?

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,646
35,981
Habari!
•Trafiki wanachukua pesa mchana kweeupe kwenye madaladala na Bajaji.
• polisi wa doria za pikipiki (tigo) nao wanachukua rushwa mchana kweeupe bila woga kutoka kwa bodaboda.
•Mahakamani nako rushwa iko waziwazi.
•Ofisi za halmashauri rushwa nje nje. Nenda pale depo ya Jiji karibu na Kamata Kariakoo kajionee rushwa ya waziwazi.
• Wakala za serikali rushwa nje nje. Hutoi pesa hupati tenda.
•Ofisi karibu zote zinazohusika na kusajili biashara rushwa waziwazi.
Imefika wakati polisi vituoni ukiwa na pesa hata ufike saa nne usiku utapata dhamana na kama huna Hela hupati dhamana hata wiki mbili wataendelea kukushikia na wakihakikisha huna pesa au ndugu huna watakupeleka mahakamani au kukuachia.
Sasa hii taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa iliundwa ili kupunguza au kuondoa rushwa?
Au iliundwa ili tumhadae beberu kuwa misaada yake iko salama?
 
Back
Top Bottom