Je, taarifa ya ndege ya Air Tanzania kuanguka ziwani Victoria ni ya kweli?

Najiandaa kwenda airport Dar kumpokea mgeni wangu napigiwa simu sasa hivi ndege iliyokuwa iwalete Dar imeanguka ziwa Victoria, uokowaji unaendelea.

Mwenye taarifa zaidi tujurishane maana Jiji zima la Dar na Zanzibar halina umeme.

=====
UPDATE ;
======

Ndege za Air Tanzania ziko salama hakuna ajali yoyote.

Ila leo asubuhi, Mamlaka ya viwanja vya ndege Uwanja wa Bukoba waliendesha zoezi la kuonyesha utayari endapo ajali ikitokea. Zoezi hilo ni la kawaida na ufanyika mara kwa mara katika viwanja vingi duniani na ni kati ya taratibu zilizo ndani ya sheria za usafiri wa anga wala halina madhara yoyote.

Poleni kwa taharuki iliyojitokeza.
Mkuu Mimi Nipo Airport hapa Naondoka na Air Tanzania Kwenda Dar Pako Shwali tu.
 
Hii ni taarifa ya kweli, wageni wangu wapo airport Mwanza walikuwa wapande ndege hiyo kuja nayo Dar.

Wametangaziwa hivyo hapo airport, ni taarifa nisizo na chembe ya shaka nazo.

Sijui kuhusu vifo, naambiwa uowokowaji ziwani unaendelea.
Aisee
 
Back
Top Bottom