Je,taaria mbaya ya Siri ya utendaji kazi anayoandikiwa mtumshi wa umma na Bosi wake inamadhara?

Mshua's

JF-Expert Member
May 22, 2013
801
545
Habari zenu Wakuu! Naomba kujuzwa kama taarifa mbaya ya siri anayoandikiwa mtumishi wa umma na bosi wake inaweza kusababisha madhara kwa mtumishi husika? Hii ni kwa sababu nimekuwa na bosi ambaye haridhishwi na utendaji wangu wa kazi tangu aje kituo hiki ninachofanyia kazi wakati kuna mabosi kama wanne waliopita wamekuwa waki "appreciate" utendaji wangu wa kazi. Sasa, amekuwa akinitishia kuwa ataniandikia taarifa mbaya ambayo haitaniwezesha kupata senior positions au uongozi wa kituo chochote katika idara yangu ninayofanyia kazi. Naomba kwa yeyote mwenye uelewa atufahamishe ili tuondokane na kubabaishwa na hawa wazee wanaokaribia kustaafu katika utumishi wa umma. Kama ni ishu nyeti sana ambayo anaona si vizuri kuiweka hapa hadharani, naomba ani PM. Mimi ni Mtumishi wa umma (Serikali Kuu) na nina uzoefu wa takribani miaka 8 lakini sijapata kujua huwa wanaandika nini mabosi wetu kwenye hayo mafaili ambayo huyatunza kwenye makabati yaliyomo kwenye ofisi zao. Na huwa wanatutishia kwa kusema ofisi yote ndio imebebwa na hayo makabati. Magari, furniture, na mambo mengine yote huwa ni bla bla tu! Naomba kuwasilisha
 
Serikalini hamfanyi perfomance appraisail?

Na mkifanya huwa mnajadiliana na bosi wako?

Kama bosi kakuandikia kitu sicho si unakataa?
 
Mnatumia OPRAS?...


Tuliwahi kutumia OPRAS kupima utendaji kazi mara 1 tu ilikuwa mwaka 2009, huyu bosi hakuwepo. Huu utaratibu haujatumika tena na hawakutujulisha ni kwa nini hawakuendelea kutumia huo utaratibu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom