Je, sukari imeshuka bei? Kama mimi ningekuwa Rais ningesema hivi.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, sukari imeshuka bei? Kama mimi ningekuwa Rais ningesema hivi....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Big Dady, Mar 7, 2011.

 1. B

  Big Dady Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati wa hotuba yake mwishoni mwa mwezi wa pili Rais alieleza mtizamo wake juu ya kupanda vitu bei. Nasema ulikuwa ni mtizamo wake kwa sababu aliyosema hadi sasa hayajatekelezwa. Hebu tuangalie aliyosema kuhusu bei ya sukari. Rais alionesha kutoridhishwa na bei ya sukari kwani iko juu mno. Kwa maoni yake alisema bei ya sukari haitakiwa kuwa zaidi ya shs. 1,700.00. Kwa jinsi alivyotamka NILIKATA TAMAA, maana haikuonsha kama alikiongea alikuwa na dhamira nacho hasa, matokeo yake hakuna chochote, watu tunaendelea kuumia, kufulia, n.k.

  Kama mimi ningekuwa ndiye BOSS wa nchi hii, ningetoa kauli ambayo kina kona ya nchi hii watu wangesema 'LEO MWANAUME KAONGEA'. Ningesema hivi, 'KUANZIA TAREHE 10 MWEZI WA TATU HAKUNA KUUZA SUKARI ZAIDI YA SHILINGI ELFU MOJA NA MIATANO. NATOA SIKU KUMI ZA KUMALIZIA KUUZA WALE WANAODAI WALIIPATA KWA BEI KUBWA. NAFUNGULIA MILANGO YA KUINGIZA SUKARI KUTOKA ZAMBIA, MALAWI, KENYA, N.K. NAAGIZA WAKUU WA MIKOA, WILAYA, WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI, POLISI NA WOTE WENYE MAMLAKA KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA AMRI HII. SUALA LA VIWANDA VYA SUKARI HAPA NCHINI NAAGIZA WAZIRI WA WIZARA HUSIKA KUFUATILIA.

  Hapo wana JF nchi nzima ingezizima kwamba leo MWANAUME KALONGA, lakini kwa ile kauli dhaifu, tutaendelea kupigishwa kwata ya ugumu wa maisha kila siku. AMA KWELI SASA NI MAISHA MAGUMU KWA KILA MTZ.
   
 2. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Duh!.....gongo kweli haina mesheni1
   
 3. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  gongo tena
   
 4. J

  John10 JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pointi yako ni Nonesense. Utawala wa TZ upo ktk free market. Rais hana mamlaka ya kupunguza sukari. Also, hatupo ktk mfumo wa Ujamaa kama tulivyokuwa na Dictator Nyerere.
   
Loading...