Je, suala la kujaza abiria haliwahusu mwendo kasi na daladala?

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,409
13,259
Baada ya ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1 kule Arusha nimesikia mmiliki wa shule amekamakwa kwa kuzidisha watu 8 katika lile basi. Sasa nauliza mamlaka husika, je hili suala la kujaza abiria kupita uwezo au siti zilizopo katika mabasi halihusu mabasi ya mwendokasi na daladala? Maana kwa sasa mabasi yanayoongoza kwa kujaza abiria tena katika hali ya kushonana mno ni mwendokasi na daladala hasa nyakati za asubuhi na jioni. Je na wao wamiliki wao watakamatwa ajali ikitokea na kufa watu wengi? Maana mabasi kama mwendo kasi yale mafupi na marefu, Mungu apishilie mbali siku ya siku ikitokea itakuwa maafa! Kwa sasa hakuna anayeona au kujali mapaka litokee tukio maana hii ni nchi ya matukio. Kama hakuna tukio basi huwa hakuna tatizo ingawa ishara na dalili ya tatizo huwa wazi.

Mabasi karibia yote ya wanafunzi hubeba wanafunzi wengi zaidi ya siti kwakuwa wanafunzi wenyewe huwa na size ndogo ndogo hivyo siti moja wanaweza kukaa wawili na huwa yanapita mbele ya askari lakini huwa hayasumbuliwi wala kukaguliwa. Sasa limetokea hili balaa kila askari ameibuka na amri zake lakini wakati huo huo mengine kama hayo niliyoyataja yanaachwa. Hili la Arusha limepita, je tunasubiri jingine ndipo tujue kuwa avumaye ni papa kumbe na wengine wamo?
 
Una point, tatizo ni changamoto ya usafiri wa mjini hasa Dsm, daladala huwa wanajitetea kuwa hawakimbii sana na safari zao ni za karibu karibu.
 
Jibu lako ni kama mada ya bashite vs wenye vyeti feki.
Una point, tatizo ni changamoto ya usafiri wa mjini hasa Dsm, daladala huwa wanajitetea kuwa hawakimbii sana na safari zao ni za karibu karibu.
 
Back
Top Bottom