Je Stanbic na Mkombozi wana kosa kuruhusu cash withdrawal ya zaidi ya 10million?

beko

Senior Member
Apr 11, 2011
188
225
Kuna swala la kujiuliza kuhusu kiwango cha CASH mteja wa bank anaruhusiwa kudraw kutoka bank, kuna watu humu wanasema ni million 10, mimi nasema hapana, kwani in practice watu wengi wanafanya miamala ya cash zaidi ya 10million, hapa inabidi bankers watupe sheria hiyo inasemaje, kwani kama mtu anataka kudraw cash kwenye account yake kwanini awekewe kiwango? mbona mtu akitaka kudiposit cash kiwango chochote hazuiwi? iweje akitaka kudraw azuiwe?. Chukulia mfano watu wanaofanya biashara za Cash Zaidi kama vile minadani, n.k wao watahitaji cash kiasi kikubwa sana, pia watu wanaonunua madini migodini, huwa wanabeba cash kubwa, kama 10million ndio kiwango cha juu, je wangeweza kufanya biashara?. Ni vizuri watu tuelewe ni kiwango gani cha juu cha cash withdrawal kinaruhusiwa na sheria za mabenk? Please mwenye hiyo sheria atujuze.
 

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,202
2,000
Binafsi nimewahi kufanya kazi bank na kwa muda wote niliokuwa pale sikuwahi kuiona wala kuisikia hiyo sheria. Jambo ninalofahamu, kwa kiwango fulani cha kuchukua, kisheria, mteja anatakiwa kuwa na escort na hii ina-apply zaidi kwa cheque za serikali(though not exclusively to government payments alone)! Mathalani, ukiwa umeenda bank na cheque ya 25 million (sheria inataja kiwango kidogo zaidi) na unataka kuchukua, Telller haruhusiwi kulipa hadi aone muhuri wa kituo cha polisi na ajiridhishe kiwamba polisi yupo. Teller asipofuata utaratibu huu na kwa bahati mbaya payee akakabwa mara baada ya kutoka bank, Teller hapo una kesi ya kujibu...

Under money laundering prevention and control, the receiving bank ndie yupo more responsible than the paying bank. I mean, mathalani Anna Tibaijuka ame-draw ile 1.6 billion (no offense), na ameenda ku-deposit CRDB Bank... it doesn't matter kama ni kwenye a/c binafsi au ni hiyo ya shule kama anavyosema... hapo CRDB ni LAZIMA wafuatilie kufahamu uhalali wa hiyo pesa... inatoka wapi na kwa biashara ipi!

Tukija suala la Rugemalila na Mkombozi Bank... Rugemalila ni mteja wa Mkombozi Bank na kama ni mteja wao maana yake ni kwamba hawana mashaka nae... huwezi kusema haruhusiwi kutoa pesa... hakuna kitu kama hicho! Kinachotokea mara nyingi, depending na bank yenyewe, kuna amaount kui-draw unatakiwa kutoa three days notice! Hata hivyo si kwamba hauruhusiwi moja kwa moja kutoa at short notice, NO... unaruhusiwa bali utakumbana na charges za kutolea hiyo amount in addition to any existing withdrawal charges (if available)!

Technically, hii charge sio kwamba ni adhabu, la hasha! Mabenki hayakai na pesa nyingi kwenye matawi... kila tawi lina amount ambayo wanaruhusiwa kukaa nayo overnight kisheria (to minimize the risk of robbery)... hii inaitwa Branch Cash Limit na lazima Branch Manager ahakikishe ana-comply na cash limit ya tawi lake! Kama Branch cash limiti ni 500 million na ukalala na 1.5 billion halafu ukaibiwa... Meneja/custodian una kesi ya kujibu... hapo unaambiwa ulifanya makusudi na hivyo kushirikiana na majambazi....

Back to the issue! Sasa, assume cash limit ya Branch X ni sh. 1 billion, na wewe unakuja at short notice na kutaka kutoa 3 billion (ambayo hapo haipo)! Katika mazingira kama hayo ni kwamba unailazimisha benki ifanye emergence cash transit ili waweze kukulipa!
 

Faridi

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
672
250
Sheria inaweza kuwepo lakini inafahamika kuna sheria nyingi zinajulikana pale kuna jambo limetokea.Kuna sheria nyingi hazifuatwi na zengine hazitekelezeki inabidi zifumbiwe macho, vipi kwa hizi pesa zetu za madafu na mfumuko wa bei benki ikaweka limit ya 10,000.00 hata kama sheria ipo haitekelezeki maana pesa yetu haina thamani lakini kuna wakati benki inataka kutumia general knowledge na kujiuliza pale mtu anatoa cash labda pesa nyingi saana na kumshauri ahamishe kwa kutumia Bank Transfer au kuchukua bank Cheque/Draft.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom