Je, spare za BMW MIN COOPER zinapatikana kirahisi?

Ufwandunkanye

Senior Member
Jan 7, 2017
123
192
Habari zenu wakuu.

Naombeni msaada wenu kujua kama upatikanaji wa spare za BMW MIN ni rahisi kama wa gari nyingine za Toyota. Ninavutiwa sana na gari hii, nafikiri siku yoyote naweza kutimiza ndoto ya kuwa nayo, lakini naweza badili maamuzi kama upatikanaji wa spare zake kwa ajili ya service ni mgumu.

Naomba kuwasilisha.

BG389050_05b4df.jpeg
 
Kupatika kwa wingi kama toyota hapana. Ila zipo. Wakati mwingine inabidi uagize nje. Hii ni kwa magari mengi ambayo siyo ya Japan.
 
Siku hizi hakuna hofu ya spea
Unatuma kadi dubai au south africa unalipa Dhl bada siku tatu unaletewa spare yako
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Siku hizi hakuna hofu ya spea
Unatuma kadi dubai au south africa unalipa Dhl bada siku tatu unaletewa spare yako
Mkuu msaada hapo jinsi ya kuagiza, nateseka sana kununua kariakoo spare hata wiki haimalizi ishakufa
 
Mkuu msaada hapo jinsi ya kuagiza, nateseka sana kununua kariakoo spare hata wiki haimalizi ishakufa
Google dealers wa spare parts south africa na dubai utawapata wengi tu
Tuma copy ya kadi part namba au jina la kifaa na picha
Watakutumia proforma invoice,ipeleke Dhl watakupa gharama zao za kuleta au kama supplier kaweka gharama za dhl vizuri pia
Walipe dhl pesa,wao watamlipa supplier na kukuletea mzigo wako
 
Sasa hivi hata ukiagiza Tesla wala hauwazi spare dunia ishakua kama kijiji.....kuna jamaa yangu yupo bunda anatumia ford F15 na spare anapata kama kawa...
 
Google dealers wa spare parts south africa na dubai utawapata wengi tu
Tuma copy ya kadi part namba au jina la kifaa na picha
Watakutumia proforma invoice,ipeleke Dhl watakupa gharama zao za kuleta au kama supplier kaweka gharama za dhl vizuri pia
Walipe dhl pesa,wao watamlipa supplier na kukuletea mzigo wako

Jinsi ambavyo wewe mwenyewe hujawahi kuagiza spares online umeishia tu kutoa maelezo ya ujumla kama vile huyo msela hapajui Google.
 
Google dealers wa spare parts south africa na dubai utawapata wengi tu
Tuma copy ya kadi part namba au jina la kifaa na picha
Watakutumia proforma invoice,ipeleke Dhl watakupa gharama zao za kuleta au kama supplier kaweka gharama za dhl vizuri pia
Walipe dhl pesa,wao watamlipa supplier na kukuletea mzigo wako
Vitu Kama hamvijui msiwe mnavitolea maelezo, Tangu lini dhl akapokea malipo ya kununua item? Dhl Ni msafirishaji tu sana sana atadai hela ya kusafirishia na hiyo utachajiwa kabla hujatuma mzigo.
Umeunga unga taarifa za Google halafu unakuja kumshauri mtu, ilhali hata hujawahi kufanya hicho kitu.

Sent
 
BMW sio kama Toyota unabadili kitu baada ya mwezi unasikia kinagonga tena ni magari magumu sana sio kidogo na mpaka kitu kiharibike imetembea...
 
  • Thanks
Reactions: Lee
We nunua kitu roho inapenda, spea zipo nyingi na genuine mtandaoni ingia beforward, agiza watakuletea, haya maspea ya kariakoo mengi ni fake na mengine ni used yameshachoka.
 
Back
Top Bottom