lufunyo
Member
- Oct 29, 2010
- 70
- 2
Mimi ni mmoja wa wafuasi wa kupigania haki za wanyonge na kupambana na ufisadi Tanzania.>nilifurahishwa sana na Bunge lililopita na jinsi lilivyoendeshwa. Lakini kinachonikwaza mpaka leo ni namna michakato yote ya mijadala ilivyoisha. Hakuna suluhisho hata moja lililofikiwa ili kuokoa rasilimali zetu kutoka mikononi mwa mafisadi. Na hii yote imesababishwa na udhaifu wa Mh. Sitta kushindwa kusimama kidete kutetea hoja ya mijadala bungeni badala yake ameendelea kunyenyekea uanachama na ujumbe wa chama chake. Je Sitta alikuwa na lengo mahsusi ya kuruhusu mijadala ile bungeni au ni udhaifu wake wa kushindwa kuzuia mijadala kama ile ndiyo kulipelekea kuibuka kwa hoja zile? kama ni ndiyo kwanini alirudi Kwenye chama kuomba misamaha ili asifutwe uanachama? mi bado simwelewi vizuri naomba michango yenu wanaJF.:sorry: