Elections 2010 Je Sitta Kuruhusu mijadala ya Ufisadi Bungeni ni Ujasiri Au Udhaifu..

lufunyo

Member
Oct 29, 2010
70
2
Mimi ni mmoja wa wafuasi wa kupigania haki za wanyonge na kupambana na ufisadi Tanzania.>nilifurahishwa sana na Bunge lililopita na jinsi lilivyoendeshwa. Lakini kinachonikwaza mpaka leo ni namna michakato yote ya mijadala ilivyoisha. Hakuna suluhisho hata moja lililofikiwa ili kuokoa rasilimali zetu kutoka mikononi mwa mafisadi. Na hii yote imesababishwa na udhaifu wa Mh. Sitta kushindwa kusimama kidete kutetea hoja ya mijadala bungeni badala yake ameendelea kunyenyekea uanachama na ujumbe wa chama chake. Je Sitta alikuwa na lengo mahsusi ya kuruhusu mijadala ile bungeni au ni udhaifu wake wa kushindwa kuzuia mijadala kama ile ndiyo kulipelekea kuibuka kwa hoja zile? kama ni ndiyo kwanini alirudi Kwenye chama kuomba misamaha ili asifutwe uanachama? mi bado simwelewi vizuri naomba michango yenu wanaJF.:sorry:
 
Mimi nadhani sio udhaifu wa kushindwa kusimamimia mijadala. Sitta alijipambanua kama mtu mwenye uwezo wa hali ya pekee katika kuruhusu mijadala yenye manufaa kwsa taifa na naamini kuwa alidhamiria kuhakikisha taifa haliendelei kuibiwa na wachache. Tatizo kubwa lilikuwa ni kutaka kukata tawi la mti aliokalia (CCM) ambalo viranja wake wakuu ndio walio mstari wa mbele kuwafisadi watanzania. Hili ndilo liliopelekea kutaka kutimuliwa uanachama. Hapa ndipo udhaifu ulipo na ndio maana mimi naamini hata kama leo akitokea malaika kupambana na udhaifu wa CCM kama atakuwa ndani ya CCM basi hatafanikiwa, maana kwa sasa mafisadi ndio wenye chama.
Kimsingi aliamini ataweza kuutafuna mfupa lakini looh!!! Akajikuta anazidiwa janja na wenye chama. Pole bwana Six ila naamini bunge la 9 chini yako litakumbukwa kwa chemchem ya vuguvugu la mabadiliko Tanzania!!! Bravo Six
 
Sitta hakuwa anajisimamia mwenyewe. Ndio sababu anachezewa na kila mmoja. Alichezewa na wapinzani sasa anachezewa na CCM. Labda hii ndio lugha tamu kwa wana CCM
 
Mimi nadhani sio udhaifu wa kushindwa kusimamimia mijadala. Sitta alijipambanua kama mtu mwenye uwezo wa hali ya pekee katika kuruhusu mijadala yenye manufaa kwsa taifa na naamini kuwa alidhamiria kuhakikisha taifa haliendelei kuibiwa na wachache. Tatizo kubwa lilikuwa ni kutaka kukata tawi la mti aliokalia (CCM) ambalo viranja wake wakuu ndio walio mstari wa mbele kuwafisadi watanzania. Hili ndilo liliopelekea kutaka kutimuliwa uanachama. Hapa ndipo udhaifu ulipo na ndio maana mimi naamini hata kama leo akitokea malaika kupambana na udhaifu wa CCM kama atakuwa ndani ya CCM basi hatafanikiwa, maana kwa sasa mafisadi ndio wenye chama.
Kimsingi aliamini ataweza kuutafuna mfupa lakini looh!!! Akajikuta anazidiwa janja na wenye chama. Pole bwana Six ila naamini bunge la 9 chini yako litakumbukwa kwa chemchem ya vuguvugu la mabadiliko Tanzania!!! Bravo Six

Hapo chacha. no comment at oll..........
 
Sitta ni jasiri ila kikwazo ni mfumo wa CCM kwamba wanaujasiri wa kusimamia uozo.
 
mimi ni mmoja wa wafuasi wa kupigania haki za wanyonge na kupambana na ufisadi tanzania.>nilifurahishwa sana na bunge lililopita na jinsi lilivyoendeshwa. Lakini kinachonikwaza mpaka leo ni namna michakato yote ya mijadala ilivyoisha. hakuna suluhisho hata moja lililofikiwa ili kuokoa rasilimali zetu kutoka mikononi mwa mafisadi. Na hii yote imesababishwa na udhaifu wa mh. Sitta kushindwa kusimama kidete kutetea hoja ya mijadala bungeni badala yake ameendelea kunyenyekea uanachama na ujumbe wa chama chake. Je sitta alikuwa na lengo mahsusi ya kuruhusu mijadala ile bungeni au ni udhaifu wake wa kushindwa kuzuia mijadala kama ile ndiyo kulipelekea kuibuka kwa hoja zile? Kama ni ndiyo kwanini alirudi kwenye chama kuomba misamaha ili asifutwe uanachama? Mi bado simwelewi vizuri naomba michango yenu wanajf.:sorry:
yeye kama spika alitimiza wajibu wake, ambao hatukutimiza wajibu wetu ni sisi wananchi ambao wabunge ni wawakilishi wetu. Hatukuandamana kumuunga mkono sitta na timu yake, hali amabyo ingeifanya serikali kuchuku hatua kali. Badala yake baada ya kuona kuwa wananchi hatuchukui hatu za kufaa mafisadi wakamshughulikia yey na timu yake huku sisi tukishuhudia.
 
Ivi imagine kama angekuwa Msekwa pale kama mngejadili Richmond
Issue ni CCM but Mzee Six aminia
 
Sitta alionyesha ujasiri na kutimiza ile ahadi yake ya standard and speed.Na ukweli aliweza kuruhusu mijadala mizito ambayo iliruhusu uma kuweza kujua hujuma tunayofanyiwa na mafisadi.Hivyo tatizo ni CCM.
 
Huo ulikuwa ni ujasili na ataendelea kukumbukwa daima!the truth shall prevail!!
 
I suppose kilichommaliza Sita ni danadana na chenga nyingi akiwa golini. When the strategic window of opportunity open ( and it does once) one got to exploit optimally. Six had to finish business early enough, kubla wachawi hawajamshitukia na kujipanga. Imebaki ningejua... Any way he achieved what he invested (mtaji kiduchu, faida kiduchu) and now is paying the price. He had the resource and opportunity but could not score.
 
Back
Top Bottom