Je, Sirro ana sifa, weledi na uzoefu wa Ubalozi?

lord atkin

Senior Member
Sep 30, 2018
197
683
Hivi balozi zetu huko nje ni kichaka/jalala la wastaafu na watendaji wasioendana na kasi ya mabadiliko kama anavyodai Mheshimiwa Rais kuwa Sirro ameshindwa kuendana na kasi ndani ya jeshi la polisi? Kama ameshindwa kuendana na kasi ndani ya polisi ataendana na kasi ubalozi?

Uzoefu unaonesha vyeo vya ubalozi hivi karibuni vimekuwa vikitolewa kama zawadi Kwa wastaafu, au vikitumika kuwapooza viongozi walioondoshwa kwenye nyadhifa fulani au kuwatupa wanasiasa tunaotaka kuwatoa kwenye mainstream politics.

Hii si sawa kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi na diplomasia yetu ya uchumi.
 
Kuna vyeo mtu akifikia huwa anahudumiwa na Serikali maisha yoye. Huduma huwa ni;
1. Kubadilishiwa gari kila baada ya muda fulani
2. Kuwekewa mafuta kila mwezi
3. Kulipwa mshahara au sehemu ya mshahara kila mwezi
4. etc

Sasa mstaafu wa hivi, ni bora awekwe sehemu ili anacholipwa kifanye kazi. Maana kwa kuwekwa sehemu husika, atalipwa kile kile ambacho angeliwa kama angekuwa nyumbani tu... So kiuchumi, ni bora umpe kazi ili akitumikie kile anacholipwa badala ya kumuweka mwingine ambaye utamlipa tena huku mstaafu akilipwa pia
 
Swali ni Je ana sifa za anapowekwa? Unaweza ukafikiri unaokoa pesa lakini kumbe Kwa kuweka incompetent ubalozini ukaingia hasara kubwa Kwa kuzorota diplomasia kuliko ungemnunulia hilo gari jipya akalee wajukuu au peleka muswada bungeni punguza marupurupu yasiyo na ulazima yabaki ya muhimu tu
 
Ni sawa ulichokisema, lakini ukumbuke nimesema unamlipa mtu hata akiwa yupo nyumbani kalala kila siku..!! Sasa kumuacha yeye na kumuweka mtu mwingine, maana yake unaingia gharama ambazo hukutakiwa.

Kutokuwa na sifa, kunazibwa na mishahara miwili ya kuwalipa watu wawili, mstaafu na mteuliwa ambaye siyo mstaafu..!!
 
UBALOZI ni vyeo vya kijeshi/kijasusi. Anaweza tena kwa 100% tunawaambia hapa 90% ya mabalozi wetu wote ni kutoka vyomba vya ulinzi na Usalama.

Huku SADC nchi moja tu ndio imepata mtu ambaye sina hakika kama ni ASKARI (POLEPOLE) Ingawa anaweza kuwa TISS.

Hivyo vyeo vinatoka kwa sababu maalumu, kuangalia uhusiano wa nchi na nchi, ushirikiano wetu upoje na kama kuna hali ya tahadhari juu ya ushirikiano wetu. Hivyo wanaotoka kwenye hizo kada huwa ni haraka kujua.
 
Huo ujasusi wao umesaidia nini kwenye nchi yao iliyochoka ?
 
nimesema unamlipa mtu hata akiwa yupo nyumbani kalala kila siku..!! Sasa kumuacha yeye na kumuweka mtu mwingine, maana yake unaingia gharama ambazo hukutakiwa.

Kutokuwa na sifa, kunazibwa na mishahara miwili ya kuwalipa watu wawili, msfaatu na mteuliwa ambaye siyo mstaafu..!!
Kwani ubalozini halipwi mshahara ?
 
Sirro ndio syahiki hasa kwakuwa ni shushushu na ndio sifa za mabalozi
 
Hivi balozi zetu huko nje ni kichaka/jalala la wastaafu na watendaji wasioendana na kasi ya mabadiliko kama anavyodai Mheshimiwa Rais kuwa Sirro ameshindwa kuendana na kasi ndani ya jeshi la polisi? Kama ameshindwa kuendana na kasi ndani ya polisi ataendana na kasi ubalozi?

Uzoefu unaonesha vyeo vya ubalozi hivi karibuni vimekuwa vikitolewa kama zawadi Kwa wastaafu, au vikitumika kuwapooza viongozi walioondoshwa kwenye nyadhifa fulani au kuwatupa wanasiasa tunaotaka kuwatoa kwenye mainstream politics.

Hii si sawa kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi na diplomasia yetu ya uchumi.
Kwa bongo hapa,hivi vyeo,ubalozi,RC,UDC,wanapewa watu reject kwenye system,waende wakastaafie huko,siro siyo mwanadiplomasia,hajuhi chochote kuhusu diplomasia,mkuu wa nchi hamtaki,anapewa ubalozi akamalizie miaka yake ya kustaafu tu,yaani ccm wamechoka hawajuhi wafanye nini!hawana plan,I wish these people could drop and die.
 
Sirro ndio syahiki hasa kwakuwa ni shushushu na ndio sifa za mabalozi
Ubalozi ni zaidi ya ushushu, huko ushushu wa kazi gani?
Dunia ya sasa kinacholipa ni diplomasia ya uchumi.
Huyu alishazoea dezo, kujengewa ma lodge na ma Rpc wa mikoa na kupelekewa mahindi kwenye kiwanda chake cha kusindika unga.

Hajui chochote zaidi ya kuihujumu chadema na kutumia madaraka yake kujinufaisha.

Ubalozi amepewa kama shukrani ya kuitetea ccm na si vinginevyo
 
UBALOZI ni vyeo vya kijeshi/kijasusi. Anaweza tena kwa 100% tunawaambia hapa 90% ya mabalozi wetu wote ni kutoka vyomba vya ulinzi na Usalama.

Huku SADC nchi moja tu ndio imepata mtu ambaye sina hakika kama ni ASKARI (POLEPOLE) Ingawa anaweza kuwa TISS.

Hivyo vyeo vinatoka kwa sababu maalumu, kuangalia uhusiano wa nchi na nchi, ushirikiano wetu upoje na kama kuna hali ya tahadhari juu ya ushirikiano wetu. Hivyo wanaotoka kwenye hizo kada huwa ni haraka kujua.
Polepole ni bora mara 200 kwa Nyankoro Sirro.
Hawa maafande hawana lolote kwa ubalozi.
Rejea mtu kama Mangu, hajawahi fanya lolote hadi amerudishwa nchini.
 
Sirro hajashindwa kuendana na kasi ya mama. Isipokuwa labda mama kashindwa kuendana na kasi ya sirro.

Ikumbukwe mama aliipokea nchi chini ya sirro baada ya magu kufa ikiwa salama bila tishio lolote la uhalifu, panya road wala ugaidi.

Ni sirro ndio aliingia mstari wa mbele kutembeza kichapo kwa magaidi kule kibiti na akatuliza kabisa.

Kwa mara ya kwanza tuliona majeshi yetu yakiwa kitu kimoja chini ya mwenyekiti wao mabeyo. Yaani sirro na mabeyo waliishi kama brothers tofauti na huko nyuma uhasama uliokuwepo kati ya haya makundi mawili.
 
Umeota magego unamdharau Rais Samia kiasi hiki? Kweli Sukuma Gang mnamchukia sana Rais Samia
 
Binafsi naona tatizo ni kubwa kuliko hata kulipwa marupurupu baada ya kustaafu. Kuna haja haya mambo yakaangaziwa upya, Hawa jamaa wanaolipwa mishahara mine na mazagazaga mengi wakiwa madarakani, isitoshe wakistaafu, wanapata kitu kama pisho Nene tu. Wakati watumishi wa umma waliowengi wanalipwa pesa njiwa na ukistaafu hiyo pension Yako ni ya manati.

Tatizo kubwa Kwa upande wangu ni athari kwenye utendaji wao wa kazi kabla ya kustaafu, mkuu wa majeshi au IGP atajitahidi ajikombe Kwa Kiongozi wa nchi ili kujihakikishia nafasi ya uteuzi pindi anapostaafu. Kwamaanahiyo, hawezi kuutekeleza majukumu yake Kwa weledi asipokua makini, mustakabal na hatma yake baada ya kustaafu itakua inaongoza maamuzi yake kazini.
 
Huo ujasusi wao umesaidia nini kwenye nchi yao iliyochoka ?
Pamoja na kuchoka unakoona wewe ila TANZANIA katika nchi 10 zenye uchumi mkubwa Afrika hatukosi, hata kwa maendeleo ya kawaida Tanzania tumeziacha mbali nchi nyingi sana.

Kwa upande wa SADC nchi ambazo zimetuzidi ni SOUTH AFRICA na ANGOLA. Hizo zingine hakuna wa kutufikia, jivunie nchi yako, na kumbuka maendeleo ni vile wewe unavyoyaona, ila nakuhakikishia Tanzania ni one of the most developed country in our Continent.
 
Sasa mtu maisha yake yote alizoea kupokea na kutoa amri! Atakuwa na ubunifua gani kwa nchi! Huyu alitakiwa kustaafu na kula mafao yake.

Teuzi za aina hii, ni ushahidi tosha hii nchi ina katiba mbovu kuwahi kutokea.
 
Back
Top Bottom