Je, sio sahihi Luhanjo aende likizo kupisha uchunguzi wa kamati ya bunge?

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Naamini mojawapo ya mambo yanayotakiwa kuchunguzwa na kamati ya bunge ni kukiukwa na kuingiliwa kwa mamlaka ya bunge. Mhusika mkuu katika hili ni Luhanjo.

Kama Jairo kaenda likizo kupisha uchunguzi juu ya makusanyo yenye utata, je sio muhimu Luhanjo nae aende likizo kupisha uchunguzi kuwa aliingilia na kukiuka mamlaka ya bunge?
 
Naamini mojawapo ya mambo yanayotakiwa kuchunguzwa na kamati ya bunge ni kukiukwa na kuingiliwa kwa mamlaka ya bunge. Mhusika mkuu katika hili ni Luhanjo.

Kama Jairo kaenda likizo kupisha uchunguzi juu ya makusanyo yenye utata, je sio muhimu Luhanjo nae aende likizo kupisha uchunguzi kuwa aliingilia na kukiuka mamlaka ya bunge?


Well said!!! Big up!!!
 
Luhanjo hataenda likizo ila atastaafishwa na hii itaonekana kama rais kuchukizwa na maamuzi yake ila ukweli ni kuwa muda wake ulisha expire kitambo and he is on borrowed time..USANII KWA KWENDA MBELE.
 
Wote na mkuu wao wasanii. Hapa na kuwaendea na bakora hiz protocol zitatumaliza.
 
Nani amvike Paka Kengere? Huyu bwana aliacha madudu alipokuwa na Baba Liz1 Wizara ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa na alihama naye, ni uswahiba tu!
 
Hata uamuzi wa awali kumrejesha Jairo kazini JK nafikiri alishiriki,haiwezekani Luhanjo atoe taarifa bila bosi wake kujua,maamuzi ya JK yaliangalia upepo ulivyokwenda baada ya ya Luhanjo kuweka ishu hadaharani

Natabiri waathirika wa matokeo ya taarifa ya kamati ya bunge kufanywa kama ilivyokuwa ya Richmond
 
Ndio maana Lowassa alisema serikali haina maamuzi. Sasa nani mlitaka aseme wakati boss wao alikuwa kimya. Kwanza ingekuwa wakati wa Lowassa, wala yasingefika kwa Luhanjo. Pinda na JK wote wazito wanamuachia tu Luhanjo kufanya maamuzi. Ameyafanya, oooh kafanya vibaya, kwanza mkabila, oooh sijui nini. Gosh!
Hivi Jairo naye Mbena?
 
Luhanjo hakukosea kumrudisha jairo,kwa sababu makatibu wakuu wako chini yake na wanawajibika kwake na kwa raisi.tatizo wabunge wamegeuka watendaji.na si watunga sera na sheria,mimi nafikiri jambo la wizara ya nishati sasa lifike mwisho.
 
Luhanjo yeye alitoa taarifa Huku akijua hana lolote analopoteza zaidi ya kujiwekea mazingira mazuri ya baadae wakati atakapokuwa nje ya office ( Retired officer) By the way Muda wake wa kustaafu Ulishapita anachotakiwa kufanya ni Kuondoka tu kwenye Utumishi wa Umma!! Kwa nini anang'ang'ania madaraka? Hajui taratibu za utumishi wa Umma? after 60 you are supposed to Quit... Je Hakuna mwingine anayeiweza Kazi Hiyo?
 
Mkuu busara inataka iwe hivyo lakini sijui watoa maamuzi kama wanaiona hiyo busara!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom