Je, siku ya kwanza kutongoza/kutongozwa ilikuwaje?

Siku yangu ya kwanza kutongoza mwanamke aliyenizidi urefu.
Wakuu mitandao achaneni nayo siku
Moja nikaona pisi kali instagram nikazama DM nikamuomba namba nikasepa zangu baada ya muda nikakuta sms yake yenye namba za
Simu tu . Safari ikaanza nikampigia kama week tukazoeana ikafika kukutana sasa. Mzee tukakubaliana kukutana kasehemu akatuma text kafika na Mimi nikamwambia nimefika tukaanza kuviziana nani asimame mwenzake amuone wakuu akasimama bhana mnara wa babeli huu hapa nikajikaza wakuu nikaanza story nikamweleza kua nawish awe mpenzi wangu lakini hakunijibu kitu nilishtukia kiss la nguvu mdomoni wakuu nilihisi kama mbingu zimefunguka
 
😂😂😂mkuu kwaiyo we Ni mfupi kwake .
 
Wanasema hata uwe kauzu vipi huwezi kujamba wakati unatongoza,, ila mimi nilijamba aiseh Nashukuru ilikua in silence mode halafu haikunuka kabisa

Tupo school hapo, kuna demu ana asili ya kiarabu jina lake Latifa. Huyu mtoto tulikutana kwenye mchezo wa volleyball. Yeye na wenzake walikua hawajui so wakawa wananyanyasika sana. Mzee mzima nikawa nawatetea lakini sababu kubwa ni huyu Latifa.
Katika kujali kwangu mtoto akatokea kunielewa. Lakini mzee mzima nilikua mgumu (hip hop) sana. Kitu pekee nilikua nawaza wakati huo ni kupiga chetezo kanisani na kuishabikia Man u ya Sir Alex.

Washkaji wananiambia dogo anakuelewa lakini me sina habari domo lote limejaa gundi. Kiukweli nilikua nampenda lakini nikitaka niende nafikiria hadhi yangu na uzuri wake + mabishoo wa shule wanaomtongoza basi naishia kukata tamaa, kifupi nilijidharau sababu she was so hot shule nzima.

Wanangu wakaona isiwe tabu maana wameni push wapi nimegoma wakaamua wanisakizie. Siku moja mapindi yameisha tupo free, jamaa angu mmoja akamfuata mtoto akaja nae mimi nilikua sina habari. Ghafla nikashangaa mtoto huyu hapa, jamaa nae alivyo na mbwembwe akamwambia Latifa naomba umsikilize kwa makini ndugu yangu huyu mpe nafasi usije ukamuua bure halafu akasepa.

Huku nyuma akaacha kivumbi na hapo sasa ndo ilikua balaa, mapigo ya moyo yakaanza kwenda faster, kiswahili kikageuka kingereza kikawa hakipandi kabisa ni kama nacho kilikuja na meli. Na mtoto alivyokua anajiamini muda wote ananiangalia usoni, ukicheki macho meupe kama Selena Gomez, basi mimi nguvu ndo zikawa zinaniisha kabisa kilichofuatia hapo mpaka leo nikikumbuka hua nacheka sana

U made my day Injili ya Gheto
 
bana ee mm nakumbuka kulikuwa na dada alikuwa anaitwa Hamisa..form 2 shule 1 old mosh kilimanjaro nilikuwa nampenda sana lkn kumtongoza siwez..nikaenda kwenye dawat lake nikaandika"hamisa nakupenda sana basi tu nashindwa kukuambia"..bac kesho yake asubuh dem akasoma ile meseji..akaja mbele ya darasa akauliza n nan kaandika ile meseji..darasa karibia lote kicheko

Basi siku 1 nikamwambia jamaa angu mmoja kuwa namwelewa sana yule demu..jamaa si akaenda kuwaambia washkaj..bac washkaj wakamfata dem wakampanga then wakaja nae kwenye dawati langu..wakamkalisha..then wakazunguka duara wanampamp mtoto anielewe..sasa dem akasema"et simba mteme kwel unanipenda?"...aisee nilitoka nduki brek ya kwanza choon presha juu..yan nikikumbukaga kile kituko huwa nacheka sana
Umetishaa mzeee
 
Dah inabidi uzi uendelee.
Maana umejaa shuhuda hadi Raha hivyo ngoja na mimi niandae Riwaya yangu kuendeleza Uzi.
Ila all in all Uzi Uendelee...
 
Back
Top Bottom