Je, siku ya kwanza kutongoza/kutongozwa ilikuwaje?

Yani pamoja na udomo zege wangu enzi hizo barua nilikua naziogopa sana maana ilikua kama ku bet, ikienda halafu ikute mwanamke akutaki basi jiandae kuchezea fimbo shuleni .. Mpaka home + ushauri wa wazazi na walimu .

Naomba kukuuliza personal question.

Katika kupokea pokea barua, kama kulikuwepo vipi ulipokea barua ya mwanaume yoyote ambaye humpendi na kama ndio ulifanyaje?
nikiipokea Kama sijakuelewa nakujibu ukiendelea ndo figisu zinaanza Sasa.
Umenikumbusha secondary nilikuwa msoma barua mzuri nikiagizwa kupeleka na wakigombana lazima nikapatanishe .
 
Wanasema hata uwe kauzu vipi huwezi kujamba wakati unatongoza,, ila mimi nilijamba aiseh Nashukuru ilikua in silence mode halafu haikunuka kabisa

Tupo school hapo, kuna demu ana asili ya kiarabu jina lake Latifa. Huyu mtoto tulikutana kwenye mchezo wa volleyball. Yeye na wenzake walikua hawajui so wakawa wananyanyasika sana. Mzee mzima nikawa nawatetea lakini sababu kubwa ni huyu Latifa.
Katika kujali kwangu mtoto akatokea kunielewa. Lakini mzee mzima nilikua mgumu (hip hop) sana. Kitu pekee nilikua nawaza wakati huo ni kupiga chetezo kanisani na kuishabikia Man u ya Sir Alex.

Washkaji wananiambia dogo anakuelewa lakini me sina habari domo lote limejaa gundi. Kiukweli nilikua nampenda lakini nikitaka niende nafikiria hadhi yangu na uzuri wake + mabishoo wa shule wanaomtongoza basi naishia kukata tamaa, kifupi nilijidharau sababu she was so hot shule nzima.

Wanangu wakaona isiwe tabu maana wameni push wapi nimegoma wakaamua wanisakizie. Siku moja mapindi yameisha tupo free, jamaa angu mmoja akamfuata mtoto akaja nae mimi nilikua sina habari. Ghafla nikashangaa mtoto huyu hapa, jamaa nae alivyo na mbwembwe akamwambia Latifa naomba umsikilize kwa makini ndugu yangu huyu mpe nafasi usije ukamuua bure halafu akasepa.

Huku nyuma akaacha kivumbi na hapo sasa ndo ilikua balaa, mapigo ya moyo yakaanza kwenda faster, kiswahili kikageuka kingereza kikawa hakipandi kabisa ni kama nacho kilikuja na meli. Na mtoto alivyokua anajiamini muda wote ananiangalia usoni, ukicheki macho meupe kama Selena Gomez, basi mimi nguvu ndo zikawa zinaniisha kabisa kilichofuatia hapo mpaka leo nikikumbuka hua nacheka sana

Shukuru Mungu tu hukukutana na akina Mwajuma au Asha ndala ndefu mkuu! hao watoto wenye majina ya Latifa ni wavumilivu harufu ya ushuzi aliisikia sema aliamua kuvunga tu!
 
Nikaaanza kumkwepa kila ninapomuona naona aibu namkimbia, , bwana bwana weee siku moja huyuu hapa macho kwa macho, anataka jibu lake aseee sio kwa jasho lilee .....nilikuja kumkubalia badaee sanaa
😂😂😂.
 
Nikaaanza kumkwepa kila ninapomuona naona aibu namkimbia, , bwana bwana weee siku moja huyuu hapa macho kwa macho, anataka jibu lake aseee sio kwa jasho lilee .....nilikuja kumkubalia badaee sanaa
😂😂😂ulipata kuelewa jambo lake vyema au ulizingua
 
Back
Top Bottom