Je, siasa za upinzani zimebadilika pwani ya Kenya?

snow snow

Senior Member
Sep 12, 2014
118
88
Kushindwa kwa mgombea wa chama cha upinzani cha Orange Democratic (ODM) katika uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Msambweni, pwani ya Kenya, kumeleta maswali mengi na kuzua mihemko katika jukwaa la kisiasa nchini Kenya.

Mwaniaji wa chama cha ODM Omar Boga alibwagwa na mgombea huru Feisal Badder ambaye alipata kura 15,251 huku Omar Boga wa chama cha ODM akipata kura 10,444 kati ya wapiga kura 27,313 ambao walishiriki kwenye uchaguzi huo wa jana.

Ushindi wa Feisal Badder katika eneo bunge la Msambweni ni jambo linaloonekana kuwakera wengi katika chama tawala cha Jubilee na washirika katika uhusiano baina ya kiongozi wa upizani nchini Kenya Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta.

Itakumbukwa kwamba Naibu Rais William Ruto alimuunga mkono mgombeaji huru, Feisal Bader, katika uchaguzi huu mdogo na kwa namna hiyo anaweza kusemakana kwamba amewabwaga Raila Odinga na Rais Kenyatta kwa pamoja kuhusiana na uchaguzi huu mdogo.
 
Back
Top Bottom