Je shule hii aliyoonyeshwa mtoto wa malkia wa Uingereza inawakilisha taswira halisi ya Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je shule hii aliyoonyeshwa mtoto wa malkia wa Uingereza inawakilisha taswira halisi ya Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by everybody, Nov 11, 2011.

 1. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimeona picha hii (attached) kwenye ukurasa wa IPP MEDIA (:: IPPMEDIA) ambayo inamwonyesha waziri Kawambwa na Prince Charles wakiwa kwenye shule ya msingi Leganga huko Arumeru wakiangalia kazi za wanafunzi.

  [​IMG]

  Kwa mazingira ya shule hii nina wasi wasi kwamba huyo mtoto wa Malkia atakaporudi kwao ujumbe atakao ufikisha ni kwamba Serikali ya Tanzania imeboresha shule kwa kiwango kikubwa sana kama hatapewa nafasi ya kuona upande wa pili wa jinsi ambavyo wanafunzi wa Tanzania wanakaa chini na kusomea chini ya mwembe.Ukweli ni kwamba shule kama hii ya Leganga kwa Tanzania ni za kuhesabu. Kwanini tusiwe wawazi na kuonyesha uhalisia wa umaskini wetu. Kuficha mambo haitasaidia, serikali iache wageni wanaotoka nje waone uhalisia wa utendaji wa serikali. Taswira kama hizi ndio zinamfanya Kikwete anapata masifa huko nje kwamba anaendeleza nchi na anautendaji na utawala bora wakati matatizo kem kem tunayo.
   

  Attached Files:

Loading...