Je, shinikizo kutoka nje linahitajika ili pawepo Tume Huru ya Uchaguzi?

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,772
2,171
Ni dhahiri kwamba Tume Ya Uchaguzi iliyopo si tume huru kama misingi ya chaguzi za kidemokrasia inavyohitaji.

Mojawapo ya mapungufu ya tume yetu (NEC) ni kwamba watendaji wake wote wanachaguliwa na Rais ambaye pia
ni mmoja wapo wa wagombea. Watendaji hawa wanawajibika kwake na anaweza kuwaondoa wakati wowote ikitegemea
ameamkaje siku hiyo.

Hali hii inakihakikishia ushindi CCM na serikali haitakubali hata siku moja pawepo na Tume iliyo huru.

Mojawapo ya ushahidi kuwa tume si huru ni mambo yaliyojiri wakati wa kampeni za uchaguzi ambao unaofanyika leo. Ushahidi uko wazi jinsi ambavyo TBC ambayo ni taasisi ya serikali ilivyokuwa ikionyesha muda wote kampeni za mgombea urais wa CCM na kuvinyima vyama vya upinzani fursa hiyo.

Pia tume ilikataa kupokea malalamiko ya vyama vya upinzani kuhusu mgombea wa CCM pale alipoamuru Katibu Mkuu wa TAMISEMI apeleke pesa Hedaru za kujenga kituo cha Afya wakati huo huo kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi. Kwa kuwa wito wa kuwa na tume huru ya uchaguzi unagonga mwamba je ni wakati wa kuwepo shinikizo kutoka nje ili pawepo na Tume Huru ya Uchaguzi?

Ikumbukwe kwamba si jambo geni kwa sheria kadhaa kutungwa au kubadili sheria zilizopo hapa Tanzania kutokana na shinikizo kutoka nje.

Sote tunakumbuka jinsi ambavyo sheria ya kupambana na ugaidi ilivyopitishwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 kutokana na shinikizo kutoka Marekani.

Tumeona jinsi ambavyo watanzania walishiriki katika tukio hilo ambalo limefanyika hapa wakipelekwa marekani ili wakakabiliane na mashtaka huko.

Hata hivi majuzi Rais alipopitisha Executive Order ya kuzuia wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni waisruhusiwe kendelea na masomo baadaya kujifungua, agizo hilo liliondolewa kutokana na shinikizo kutoka nje. Hata sheria ya makosa ya mtandao na sheria ya takwimu ilipunguzwa makali kutokana na shinikizo kutoka nje.

Je, wakati umefika kwa wale wanaotaka Tume Huru ya Uchaguzi kutumia mkondo wa kuomba shinikizo kutoka nje?

Nawasilisha.
 
Naunga mkono hoja. Baada ya hili zoezi kuisha, vyama vya upinzani viwekeze kwenye agenda moja tu ya kuurejesha mchakato wa Katiba Mpya ya Wananchi ili kuondokana na hii ya mwaka 1977! Katiba ya CCM.

Kinyume na hapo, haina faida kupiga kura itakayo chezewa na wateule wa mgombea wa chama tawala.
 
Hizi ndio akili ambazo serikali inatumia fedha zake kuzipa elimu,

Yaani kila Jambo wanategemea msaada toka kwa wazungu.
 
Watanzania bado hawapo tayari kutia shinikizo wao kwa wao ili kuondoa huu ufedhuli kwani japo mwishowe Magufuli na timu yake watapelekwa The Hague lkn baada ya damu nyingi kuwa imemwagika.

Hivyo njia pekee inayofaa ni vikwazo vya kiuchumi ambavyo kwa nchi tegemezi kama hii ni miezi kadhaa tu matokeo chanya yatakuwa yameonekana.
 
Mpaka Watanzania tutakapoacha ufisi ndio tutapata tume huru, maisha ya staha na kuheshimiana.Hii tabia ya ufisi na kufikiri watu wengine wafanye yale ambayo tunatakiwa tufanye sisi wenyewe hatutafika mahali.
 
Hizi ndio akili ambazo serikali inatumia fedha zake kuzipa elimu,

Yaani kila Jambo wanategemea msaada toka kwa wazungu.
Mlijidai kutumia fedha za ndani kwenye uchaguzi kumbe mlikuwa na mipango yenu michafu, mna print karatasi nyingi kupitiliza halafu zinazobaki mnajipigia kura wenyewe, wajinga kabisa.

Kila mahali zinakamatwa kura feki, uchaguzi umekuwa wa hovyo kuwahi kutokea kwenye historia ya Tanzania.
 
Hahahaa.... Hata mshindi hajatangazwa mmeshaanza kelele za tume huru, niliwaambia humu mara nyingi Lissu hawezi kuja kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kuanzia kesho nyuzi zitajaa humu za tume huru. Vipi barabarani mmehairisha kuingia au mpaka Lissu aseme!?
 
Makosa ya hapa na pale huwa hayakosi katika uchaguzi wowote ule katika nchi nyingi.

Hata hao wazungu muwategemeao, huko kwao huwa na matatizo kadhaa katika zoezi la upigaji kura.

Jambo la msingi ni kwamba safari hii uchaguzi wa mwaka huu umegharamiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia 100.

Hivyo hao watu wa nje wamekosa cha kusema ama kushinikiza na wamebakia kutembelea vituo vya kupigia kura na kuridhika na taratibu zilizowekwa na tume wakati wa kupiga kura.

Balozi wa Marekani leo ametembelea vituo vya kupigia kura.

Jambo jingine ni kwamba hao wazungu muwategemeao, safari hii waenda kushindwa vibaya na watanzania ambao leo hii wanapiga kura kwa wingi (kumbuka wapiga kura ni milioni 29 na ushei hivi) na watakichagua chama cha mapinduzi.

Safari hii mkubali mmefeli "big time" na hakuna kisingizio cha tume huru wala kuibiwa kura.

Chadema mmekuwa mkishiriki chaguzi tangia mwaka 1995 na kitendo chenu cha kuamua kuwatumia wazungu kuikashifu serikali, taasisi ya uraisi, tume ya uchaguzi na watanzania kwa ujumla, leo mnapewa kichapo cha uhakika.

Ni kama alivyosema rafiki yangu msafisha viatu kwamba Tundu Lissu atashindwa vibaya sana uchaguzi huu.

Tungoje matokeo ya uchaguzi na maisha yaendelee.

 
Back
Top Bottom