Je, Sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu watoa huduma kupandisha bei ya huduma?

Mar 26, 2018
50
125
Habarini Wana Jamvi,

Binafsi ninasikitishwa sana na watoa huduma mbalimbali pamoja na wauzaji wa bidhaa mbalimbali kuhusu upandishaji wa Bei za huduma na vitu kiholela na bila taarifa, unajikuta leo ulipata huduma kwa Bei hii, kesho ukifika umejipanga kwa Bei uliyouziwa Jana lakini cha ajabu unaambiwa au unakuta imepanda bila taarifa.

Je, sio Haki yetu kupewa taarifa na mchanganuo wa upandaji wa Bei? Sio Haki yetu kuhoji kwanini Bei imepanda?.

Leo najikita kwenye mitandao ya simu hususani Airtel ambapo wiki iliyopita nilijiunga na kifurushi ambacho kwa miaka miwili au mitatu nyuma nilikuwa nakitumia, huwa nilikuwa napata 1GB,dkk 110,sms 250,lengo kubwa la kujiunga kifurushi hichi huwa ni data na sio dkk wala sms.

Nilitumia data yote ikaisha kwa siku ile, kesho yake nikaweka ela,lengo nijiunge Tena lakini cha kushangaza nakutana na data imepunguzwa kutoka 1GB(1000Mb) mpaka Mb 500 yaani nusu yake.

Nikajiuliza maswali,kilichobadilika Jana na leo ni nini? iweje data zipunguzwe mpaka nusu ya zilizokuwa zinatolewa? mbona hawajatoa taarifa?ilihali ma sms ya betting na michezo yao wanatuma kila siku.

Kwa wataalamu wa biashara na Sheria naombeni msaada ikiwemo TCRA,Sisi watumiaji hatuna Haki ya kuhoji haya?hatuna Haki ya kupata mchanganuo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom