Je, sheria inatambua mfanyakazi kuhamishwa Kampuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, sheria inatambua mfanyakazi kuhamishwa Kampuni

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MdogoWenu, Dec 19, 2010.

 1. M

  MdogoWenu Senior Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Thinkers,

  Nadhani katika mazingira ya utandawazi si jambo geni kampuni moja kushindwa au kuacha biashara ikaendeshwa na kampuni nyingine.

  Ili niwe specific ni kwamba kuna matukio ya kampuni kuwepo kwa miaka kadhaa halafu ghafla inabadi owner yaani mmiliki lakini biashara inaendelea kuwa ileile.

  Wanaokumbuka kulikuwa na hoteli inaitwa Sheraton. Sasa haiitwi hivyo inaitwa Move N Pick. Sina uhkika na kilichoendelea kama walibadilisha mmiliki au lilibadilika jina tu.

  Lakini kuna mahali jina linabadilika na mmiliki anabadilika.

  Mfano Celtel ilipobadilika kuwa Zaina mmiliki alibadilika lakini mikataba ya wafanyakazi ikaendelea kuwa ileile.

  Ila Zaina kuja kuwa Airtel si kwamba tu jina limebadilika. Ukweli ni kwamba walichofanya Airtel ni ku-outsource baadhi ya idara.

  ivyo utakuta mfanyakazi alikuwa idara fulani sasa anaendelea kufanya kazi zilezile lakini si mwajiriwa wa Airtel kama ambavyo ungetegemea bali sasa ni mwajiriwa wa outsource company.

  Kwa mwajiriwa kama huyu ni wazi kuwa amebadili, au amehama au amehamishwa kampuni. Hapa amehama kutoka Airtel kwenda kampuni B.

  Msaada wa ufahamu hapa ni kwamba je, sheria inatambua uhamisho kama huu?

  Je, ikitokea baada ya miezi sita kampuni B uliyohamishiwa ikaavunja mkataba wa uajiri wako, je inatakiwa ikulipe haki zako za miezi sita tu au kwa muda wote ulokuwa unafanya kazi ile.

  Naomba ufahamu.
   
Loading...