JE SHERIA INASEMAJE HAPA...ni kuua au kusababishiwa kuua..

Rog3rz

Member
Jun 21, 2012
44
26
Tukio lenyewe lilitokea hapo majira ya
asubuhi mnamo Februari 21, 1978. Ni
baada ya kuambiwa mumewe wakati
anaenda kazini kwamba akirudi asimkute
hapo nyumbani, na kama akimkuta,
atamtoa hapo nyumbani kwake uchi. Alikuwa na watoto wao wanne hapo
nyumbani. Baada ya mumewe kuondoka,
na yeye aliondoka na gari kuelekea mjini
ambapo alinunua chupa kadhaa za sumu ya
kuulia wadudu. Alipofika nyumbani kwake, aliwaita watoto
wake wote wanne chumbani kwake na
kujifungia nao ndani, kisha akawaambia
“tunaondoka” watoto wale walimuuliza,
“tunakwenda wapi?” yeye akawajibu,
“tunasafiri, lakini huko tunakokwenda hatupajui.” Aliwabusu watoto wale na wao
wakambusu mama yao na kisha
wakapeana mikono kama ishara ya
kutakiana safari njema. Baada ya tukio hilo,
aliwapa kila mmoja kikombe chenye
mchanganyiko wa ile sumu na Orange Squash na yeye akachukua mchanganyiko
huo uliokuwa kwenye kikombe na
kunywa. Baada ya kunywa mchanganyiko
huo wote walianza kutapika, kutokana na
kutapika huko, aliamua kunywa Iodine. Pia
alikunywa vipande vya chupa zilizosagwa na kujifungia katika chumba kingine. Mfanya kazi wake wa hapo nyumbani
aitwae Ramadhan na mtu mwingne
aliyetajwa kwa jina la Bibie waliwasikia
watoto wakilia huko chumbani. Baadae
kidogo alifungua mlango na kumwambia
Bibie amuoshe mmoja wa watoto wale ambaye alikuwa ni mdogo kwa wenzie
kwani alikuwa anatapika na kuharisha kisha
akarudi ndani na kujifungia katika chumba
hicho peke yake. Aliombwa na Ramadhan pamoja na Bibie
watumie simu ya pale nyumbani kumjulisha
mumewe juu ya tatizo lile lakini alikataa. Wale watoto wengine watatu nao
walianza kutapika na kuharisha na hali zao
zilibadilika na kuwa mbaya. Ramadhan
aliwajulisha majirani na walipofika, yeye
alikwenda hadi chumba cha pili alipokuwa
amejifungia na kumuuliza kama ni kitu gani kimewatokea wale watoto. Alimwambia,
“Ramadhan, naomba uniache nife na
watoto wangu, kwa sababu baba Taji
(yaani Mumewe) hanipendi.” Wote walikimbizwa hospitalini na watoto
watatu waliripotiwa kufariki lakini yeye na
mwanaye mkubwa madaktari walifanikiwa
kuyanusuru maisha yao. Taarifa ya kitabibu ilithibitisha kwamba wale
watoto watatu walifariki kutokana na
kunywa sumu, ambayo walinywesha na
mama yao. Kesi hii ni ya mwaka 1979 ya Agnes Doris
Liundi, alishitakiwa na Jamhuri kwa kosa la
kuwauwa watoto wake watatu kwa
kuwanywesha sumu hapo mnamo tarehe
21 Februari 1978 nyumbani kwake.
 
Back
Top Bottom