Je sheria inasemaje hapa..kuua au kusababishwa kuua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je sheria inasemaje hapa..kuua au kusababishwa kuua

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rog3rz, Jul 24, 2012.

 1. Rog3rz

  Rog3rz Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tukio lenyewe lilitokea hapo majira ya
  asubuhi mnamo Februari 21, 1978. Ni
  baada ya kuambiwa mumewe wakati
  anaenda kazini kwamba akirudi asimkute
  hapo nyumbani, na kama akimkuta,
  atamtoa hapo nyumbani kwake uchi. Alikuwa na watoto wao wanne hapo
  nyumbani. Baada ya mumewe kuondoka,
  na yeye aliondoka na gari kuelekea mjini
  ambapo alinunua chupa kadhaa za sumu ya
  kuulia wadudu. Alipofika nyumbani kwake, aliwaita watoto
  wake wote wanne chumbani kwake na
  kujifungia nao ndani, kisha akawaambia
  “tunaondoka” watoto wale walimuuliza,
  “tunakwenda wapi?” yeye akawajibu,
  “tunasafiri, lakini huko tunakokwenda hatupajui.” Aliwabusu watoto wale na wao
  wakambusu mama yao na kisha
  wakapeana mikono kama ishara ya
  kutakiana safari njema. Baada ya tukio hilo,
  aliwapa kila mmoja kikombe chenye
  mchanganyiko wa ile sumu na Orange Squash na yeye akachukua mchanganyiko
  huo uliokuwa kwenye kikombe na
  kunywa. Baada ya kunywa mchanganyiko
  huo wote walianza kutapika, kutokana na
  kutapika huko, aliamua kunywa Iodine. Pia
  alikunywa vipande vya chupa zilizosagwa na kujifungia katika chumba kingine. Mfanya kazi wake wa hapo nyumbani
  aitwae Ramadhan na mtu mwingne
  aliyetajwa kwa jina la Bibie waliwasikia
  watoto wakilia huko chumbani. Baadae
  kidogo alifungua mlango na kumwambia
  Bibie amuoshe mmoja wa watoto wale ambaye alikuwa ni mdogo kwa wenzie
  kwani alikuwa anatapika na kuharisha kisha
  akarudi ndani na kujifungia katika chumba
  hicho peke yake. Aliombwa na Ramadhan pamoja na Bibie
  watumie simu ya pale nyumbani kumjulisha
  mumewe juu ya tatizo lile lakini alikataa. Wale watoto wengine watatu nao
  walianza kutapika na kuharisha na hali zao
  zilibadilika na kuwa mbaya. Ramadhan
  aliwajulisha majirani na walipofika, yeye
  alikwenda hadi chumba cha pili alipokuwa
  amejifungia na kumuuliza kama ni kitu gani kimewatokea wale watoto. Alimwambia,
  “Ramadhan, naomba uniache nife na
  watoto wangu, kwa sababu baba Taji
  (yaani Mumewe) hanipendi.” Wote walikimbizwa hospitalini na watoto
  watatu waliripotiwa kufariki lakini yeye na
  mwanaye mkubwa madaktari walifanikiwa
  kuyanusuru maisha yao. Taarifa ya kitabibu ilithibitisha kwamba wale
  watoto watatu walifariki kutokana na
  kunywa sumu, ambayo walinywesha na
  mama yao. Kesi hii ni ya mwaka 1979 ya Agnes Doris
  Liundi, alishitakiwa na Jamhuri kwa kosa la
  kuwauwa watoto wake watatu kwa
  kuwanywesha sumu hapo mnamo tarehe
  21 Februari 1978 nyumbani kwake.
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Ngoja@Mtambuzi aje anaweza toa ufafanuzi wa kutosha
   
 3. Rog3rz

  Rog3rz Member

  #3
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  namsubiri kwa ham maana nimesugua kichwa cpat jib...
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,824
  Trophy Points: 280
  Kuua ni kuua tu, soma kitu inayoitwa actus reus na mens rea utagundua hakuna kitu inayoitwa kusababishwa kuua kwenye case hii.


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 5. NGOGO CHINAVACH

  NGOGO CHINAVACH Verified User

  #5
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 797
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Kasome kesi ya R v. Agnes Liundi ndiyo ina same material fact na scenario yako.
   
 6. Rog3rz

  Rog3rz Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa nimepitia vyote hvyo mlivyonielekeza cpat mwanga 2 wadau....
   
 7. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mzee hii ni pure murder, kitanzi hadi kufa. kwanza kabisa alikuwa na pre-meditated knowledge and intention to kill, alikuwa sober kabisa, pamoja na uelewa huo, alifanikisha azma yake....malice aforethought (hii iko ndani ya mens rea ya murder) hapo imenyooka, na actus reus ndo kuondoka kwenda kununua sumu, na kuwanywesha watoto wote na yeye huku akijua kuwa sumu hiyo inaweza kusababisha kifo na yeye akaridhia moyoni mwake kwamba asababishe kifo.
   
 8. Rog3rz

  Rog3rz Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashukuru sana sasa nimeanza kupata mwanga mkibwa..let me search...
   
Loading...