Je, sheria inasema ni lazima uoneshe 'Lena' unapoenda kurenew Leseni ya udereva?

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
3,444
11,941
Salaam

Kuna jambo linanitatiza nikaona nililete hapa jukwaani maana ni kisima cha maarifa.

Wiki iliyokwisha nilikwenda ku renew leseni yangu ya udereva TRA nikiwa na TIN number pamoja na leseni iliyokwisha muda wake, utaratibu ulikwenda vizuri na nikaambiwa nikalipie Bank.

Baada ya hapo nikapatiwa leseni yangu iliyokwisha pamoja na karatasi za malipo na nikaambiwa nirudi baada ya siku nne kufuata leseni yangu mpya.

Sasa kizazaa kikaanzia hapo juzi niliporudi kufuata leseni mpya kwani jamaa waliniambia ni mpaka niwape lena yangu niliyojifunzia, zoezi likasimamia hapo maana lena nitapata wapi tena maana ni mambo ya karibu miaka saba iliyopita.

Wakuu hii ndiyo sheria? Na kwa nini wasiniambie awali kabla hawajachukua pesa zangu? Na kwanini wasituambie kuwa lena ni za kuhifadhiwa (japo kwenye kumbukumbu zangu waliichukua wao miaka hiyo ndiyo nikapewa leseni ya kawaida) mpaka waseme leo? Nikikosa lena nifanyeje nipate leseni?

Nawasilisha
 
Ulipo renew mara ya kwanza ilikuwaje?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom