Je, sheria inaruhusu kumuua mtuhumiwa wa ujambazi asiye na silaha anayewakimbia Polisi?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,052
40,715
Yaani tuchukulie mtuhumiwa wa ujambazi amekamatwa na Polisi, halafu wakati anawapeleka mafichoni kwa wenzake akaanza kuwakimbia Polisi huku akiwa hana silaha yoyote na akipiga makelele.

Je, kuna uhalali/ulazima wowote wa kumpiga risasi ya mgongoni na kumuua? Je, ndugu zake wanaweza kudai fidia au ni hatua gani za kisheria wanaweza kuchukua?

Nauliza tu.
 
Mkuu kisheria ni kwamba polisi anaweza kutumia deadly force anapoona maisha ya raia au yake yapo hatarini,sasa kama mtuhumiwa anakimbia away from crime scene polisi HARUHUSIWI KUTUMIA SILAHA YA MOTO bcs hasababishi raia ya yeyote kuwa hatarini.

Ni jukumu la polisi (ndio maana wamepewa nyenzo nyingi amkamate mtuhumiwa ) sio kumpiga risasi za mgongoni but elewa tumo ndani ya shithole country haya yanatokea na hakuna kitakachotokea unless umo ndani ya ile 2%ya wateule,nkuu wa usalama wa taifa,anapigwa risasi na kuuliwa akidhaniwa ni jambazi

Dada yetu Akwilina anapigwa risasi hakuna kinachofanyika(hata ballistic test haikufanywa) na maisha yanaendelea kama kawaida.tusubirie next generations zitakazo weza kurudisha jinsi ya kuishi kwa mujibu wa kisheria.
 
Nimeuliza maana kuna taarifa nimeisima humu leo eti mtuhumiwa wa ujambazi katandikwa risasi za mgongoni na kuuwawa kisa kakimbia na hakuwa na silaha yeyote mkononi..., sasa nikashangaa..., huyo mtu hana ndugu wakafungue kesi wadai fidia ya walau bilioni hata 2, maana kukimbia sio kosa la kusababisha mtu auwawe...
 
Mi nauliza kama nimeona vibaka aina ya panya road wanaingia kwangu au kwa jirani nikiwa na mishale yangu naruhusiwa kuwadungua hata wakifa sitaletewa kesi ya mauaji?
Kwa self defense ina swii ila tatizo litakuja pale tu utakuwa mistaken kumuatack mtu ambae sio kwel mwizi km vile udhaniavyo, apo 15miaka inakuhusu. Ila apo apo hakuna RAIA anaeruhusiwa kutoa uhai wa mwenzake. Sheria ni Undefined

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani tuchukulie mtuhumiwa wa ujambazi amekamatwa na Polisi, halafu wakati anawapeleka mafichoni kwa wenzake akaanza kuwakimbia Polisi huku akiwa hana silaha yoyote na akipiga makelele, je kuna uhalali/ulazima wowote wa kumpiga risasi ya mgongoni na kumuua? Je, ndugu zake wanaweza kudai fidia au ni hatua gani za kisheria wanaweza kuchukua?

Nauliza tu.
Mahali popote duniani polisi akikuamuru kusimama unapaswa kufanya hivyo. Kwa mtuhumiwa wa ujambazi anapokiuka amri hiyo polisi anapaswa kwanza kumuonya kwa mdomo, kupiga risasi juu na kama hajatii amri hiyo polisi anaruhusiwa kutumia silaha kukuzuia kukimbia. Bahati mbaya huku kwetu, silaha kuu ya polisi ni SMG ambapo risasi yake, popote itakapokupiga madhara yake ni makubwa sana. Majambazi yanafahamu fika uwezo wa silaha hiyo na wanapaswa kuieheshimu kwa kusimama wanapoamriwa kufanya hiyo.
 
Nimeuliza maana kuna taarifa nimeisima humu leo eti mtuhumiwa wa ujambazi katandikwa risasi za mgongoni na kuuwawa kisa kakimbia na hakuwa na silaha yeyote mkononi..., sasa nikashangaa..., huyo mtu hana ndugu wakafungue kesi wadai fidia ya walau bilioni hata 2, maana kukimbia sio kosa la kusababisha mtu auwawe...
kisheria ndio wanaweza kudai ILA sio kwa nchi hii ya kwetu,wajibu wa kisheria haupo kabisa na mbaya zaidi kama haupo kwenye ile 2% ya wanaotawala nchi hii,kwa nchi za wenzetu zinazoheshimu sharia hili haliwezi fanyika maana suspect was running away kwa hiyo hakuwa threat kwa yeyote,polisi wangelazimika kuomba back up ili suspect aweze kukamatwa ,ila kama alikuwa anakimbia na silaha hapo may be deadly force ingeweza tumika maana kuna uwezekano suspect angeitumia kudhuru raia.kuishitaki serikali yetu wakati watawala ndio wanauteua majaji ni ngumu mno,ni rahisi kupata majozi ya kuku kuliko la kuishitaki serikali.
 
Mi nauliza kama nimeona vibaka aina ya panya road wanaingia kwangu au kwa jirani nikiwa na mishale yangu naruhusiwa kuwadungua hata wakifa sitaletewa kesi ya mauaji?
Kama walikuwa wanahatarisha maisha yako au ya familia yako au ya jirani yako hiyo ni self defence, hivyo utaachiwa huru ikidhibitika...
 
Mahali popote duniani polisi akikuamuru kusimama unapaswa kufanya hivyo. Kwa mtuhumiwa wa ujambazi anapokiuka amri hiyo polisi anapaswa kwanza kumuonya kwa mdomo, kupiga risasi juu na kama hajatii amri hiyo polisi anaruhusiwa kutumia silaha kukuzuia kukimbia. Bahati mbaya huku kwetu, silaha kuu ya polisi ni SMG ambapo risasi yake, popote itakapokupiga madhara yake ni makubwa sana. Majambazi yanafahamu fika uwezo wa silaha hiyo na wanapaswa kuieheshimu kwa kusimama wanapoamriwa kufanya hiyo.
Kwahiyo mtuhumiwa ameshageuka jambazi tena? Hivi maana ya mtuhumiwa ni nini? Na hata kama ni jambazi, adhabu ya kukimbia ni kifo? kwa hukumu ya mahakama ipi?
 
Back
Top Bottom