Je, Shekilango na Urafiki ndio Stendi mpya za Mabasi yaendayo mikoani?

Tipstipstor

JF-Expert Member
Nov 29, 2021
1,531
3,331
Ahlan wa sahlan

Naiomba serikali ifunge hizi ofisi uchwara zilizopo hapa maeneo ya shekilango na Urafiki. Mabasi ya mikoani yamekuwa hayaendi tena kupaki stendi ya Magufuli pale Mbezi badala yake yamekuwa yakijazana maeneo ya Shekilango na Urafiki nyakati za Alfajiri na Mchana. Najiuliza ile stendi ya mabilioni pale Mbezi imejengwa kwa ajili ya kina nani?

Wahusika mpo na mnalifumbia mamcho jambo hili.Stendi imekuwa ikikosa mapato ya getini kwa abiria wanaoingia ndani ya stendi kutokana na watu sasa kumiminika kwenda maeneo ya Urafiki na Shekilango.

Wito wangu kwa serikali ni kuhakikisha mnazifunga mara moja ofisi hizi uchwara za haya mabasi hapa Shekilango na urafiki kwani hawa jamaa wameshageuza eneo hili kuwa ni terminal
 
Nadhani OFISI na STENDI ni vitu viwili tofauti.

"Ofisi zetu zinapatikana stendi ya Magufuli, chumba namba 37".

Kitu kibaya ni pale "ofisi" zinapoifanya kampuni ya mabasi isitumie huduma za "stendi".

Kwa ufahamu wangu najua mabasi yote yanatumia huduma za stendi bila kujali wana ofisi Shekilango, Magomeni, Manzese au eneo lolote lile.

Mimi sioni ubaya maana lengo kusudiwa la kujengwa kwa stendi bado linatimizwa.

Labda tu uwe umeamua kuwafanyia UKATILI hawa watu wa usafirishaji.
 
Hoja yako ya stendi kukosa mapato naona kama haina nguvu kwa sababu abiria mwenye tiketi halipi hicho kiingilio.

Na pia ofisi za kukatia tiketi pale stendi ya Magufuli zipo sehemu ambayo unaenda bure bila kulipa hicho kiingilio.

Mkuu, au wewe ni "mpiga debe" (wale wa 'usafiri wa leo blaza') pale stendi? Samahani lakini.
 
Kwani mapato ya stand yanategemea abiria kulipia getini au. Kwani zile ofisi ndani ya stand watu wanakaa Bure. Kila bus ni lazima liingie stand na kulipia. Siyo urafiki na Shekilango Kuna ofisi za mabasi tu. Hata Mbagala, Chanika, Temeke zipo.
 
Back
Top Bottom