Je shekifu alishinda bila kutoa rushwa lushoto? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je shekifu alishinda bila kutoa rushwa lushoto?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Apr 27, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima kwako mwanajf!

  Zipo tetesi kwamba, Ndugu Shekifu aligawa rushwa katika uchaguzi mkuu wa ubunge mwaka 2010 ili apitishwe kwenye kura za maoni za ndani ya chama mpaka uchaguzi wenyewe wa jimbo. Baadhi ya watu wanadai kwamba wagombea wenzake wa ubunge kutoka chama chake waliandika barua ya pamoja na kusaini kupinga uteuzi wake (isipokuwa Balozi Mshangama). Katika hali yasiyoitarajia jina lake lilipitishwa bila ya walalamikaji kujibiwa malalamiko yao na hivyo kuleta mpasuko wa ndani ya chama. Inasemekana kuwa alitengeneza kadi feki kutoka baadhi ya maeneo (mfano. Chumbageni kata ya kwemashai).

  Lakini vilevile CDM Lushoto walitoa taarifa TAKUKURU Lushoto ya Mbunge huyu kuhusika na kugawa rushwa eneo la soko kwenye hoteli ya Mapambano, TAKUKURU walifika katika eneo la tukio na katika hali ya kushangaza hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ikiwa ni pamoja na kutorudisha taarifa yoyote ya uchunguzi kwa uongozi wa CDM Lushoto.

  Kwa mkazi wa Lushoto, wasilisha mchango wako katika suala hili
  !
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,000
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  hivi ni mgombea yupi wa CCM ambaye hakutoa rushwa? naomba unitajie mmoja tu.
  kwa lushoto hakuna kesi iliyofunguliwa so ni vigumu kuchangia chochote hapa.
   
Loading...