Je,Shamsi Vuai Nahodha anakwenda kuwa nani baada ya kupigwa chini uwaziri? Kwa maana hana jimbo.

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
0
Nauliza hivi,Vuai Nahodha anakwenda kuwa nani baada ya kupigwa chini uwaziri? Alikuwa ni waziri wa kuteuliwa na Rais sio Mbunge yaani hawakilishi jimbo lolote! Je,ataendelea kukaa hotelini? Je,ataendelea kuingia bungeni? Na kama ataendelea kuingia Bungeni atakuwa anawakilisha serikali ipi?
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
26,074
2,000
Aliteuliwa Mbunge na Rais ndiyo akapewa
Wizara yaani ni Mbunge jimbo la Ikulu
Kwanafasi ya Mbunge wa kuteuliwa ataendelea kuingia bungeni km kawa
 

kill

JF-Expert Member
May 21, 2013
1,830
0
mbona mbatia yupo bungeni amewakilisha jimbo gani maswali ya kitoto haya bado pinda
 

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
0
Aliteuliwa Mbunge na Rais ndiyo akapewa
Wizara yaani ni Mbunge jimbo la Ikulu
Kwanafasi ya Mbunge wa kuteuliwa ataendelea kuingia bungeni km kawa

Ikulu ndio jimbo gani? Kwani ikulu lina wabunge wangapi? Kwa maana yupo Mbatia,Mgimwa,muhongo nk...nataka ufafanuzi mkuu
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
26,074
2,000
Ikulu ndio jimbo gani? Kwani ikulu lina wabunge wangapi? Kwa maana yupo Mbatia,Mgimwa,muhongo nk...nataka ufafanuzi mkuu

Mkuu

Ikulu ni zile nafasi kumi za Rais kuchagua watu anaowataka kuwa wabunge
si umeona juzi Migiro kala shavu
Kuna wakina Zakia Meghji na hao ukiowataja
 

Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,712
1,225
Nauliza hivi,Vuai Nahodha anakwenda kuwa nani baada ya kupigwa chini uwaziri? Alikuwa ni waziri wa kuteuliwa na Rais sio Mbunge yaani hawakilishi jimbo lolote! Je,ataendelea kukaa hotelini? Je,ataendelea kuingia bungeni? Na kama ataendelea kuingia Bungeni atakuwa anawakilisha serikali ipi?Kwani si aliteuliwa na Rais, kwani Mbatia ni mbunge wa Jimbo gani?
 

kapongoliso

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,337
1,500
Nahodha ana jimbo la Mwanakwerekwe Zanzibar kama mwakiishi. Alitangazwa kwa usimamizi wa mtutu wa bunduki.
 

kookolikoo

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
2,624
1,500
Ni mbunge wa kuteuliwa na rais kama Mbatia, Meghji, Asha Rose Migiro n.k. Mbona hawa si mawaziri na wanaingia bungeni bila kikwazo?
 

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
0
Ni mbunge wa kuteuliwa na rais kama Mbatia, Meghji, Asha Rose Migiro n.k. Mbona hawa si mawaziri na wanaingia bungeni bila kikwazo?

Hii ni kuwabebesha watz mzigo wa kulipa kodi,hajui kuwa hii nchi ni masikini? Hyu jamaa atatua na njaa, hivi sasa nauli za mabasi yaendayo mkoani yamepandisha nauli cjui ndo maisha bora kwa kila Mtanzania?
 

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,018
2,000
Nauliza hivi,Vuai Nahodha anakwenda kuwa nani baada ya kupigwa chini uwaziri? Alikuwa ni waziri wa kuteuliwa na Rais sio Mbunge yaani hawakilishi jimbo lolote! Je,ataendelea kukaa hotelini? Je,ataendelea kuingia bungeni? Na kama ataendelea kuingia Bungeni atakuwa anawakilisha serikali ipi?
Ataendelea kuingia bungeni kama mbunge wa kuteuliwa na Rais. Kuna kasoro gani hapo?
 

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
0
Katiba iliyopo ni mbovu,kama mgimwa,muhongo,mbatia,migiro,meghi,Vuai ni wabunge wa ikulu,tufanye hesabu kidogo
6*1.2 million kwa mwezi ni sawa na 7.2m *12=86.4=86,400,000*10=864,000,000 je,ni nyumba ngapi za walimu,vituo vingapi vya afya nk
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
54,676
2,000
Someni katiba mara moja moja muelewe serikali inavyofanya kazi, ngazi zake, aina za ubunge et cetera, et cetera.

Mara ya mwisho umesoma katiba lini?
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,396
2,000
Yaani uwezi amini kumbe Vuai ni mzigo halau eti alikuwa waziri kiongozi huko Zanzibar??????
Jk ni tatizo, huyu Vuai alishindwa kwenye kinyanganyiro cha Uwskilishi huko kwa Zenji, cha kushangaza Jk kampa ubunge na uwaziri, hilo ndilo la who knows who, hayo ndii majibu yake upendeleo Ccm
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom