Uchaguzi 2020 Je, Serikali kuwa na Maduka ya kuuza Dawa za Binadamu ndiyo kuimarisha Sekta ya Afya?

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,474
8,692
Yaani sijajua how come Serikali inaanza kuuza dawa yaani inafungua maduka ya kuuza dawa.

Badala wajikite kuweka mifumo bora ya afya ikiwemo Bima wao wanakimbilia kuanzisha maduka ya kuuza dawa.

Dawa zinanunuliwa kwa kodi then zinarudi kuuzwa tena, cha kushangaza hospitali na vituo vya afya unakuta kuna panadol pekee.

Aliyetoa wazo la Serikali kuwa na maduka ya madawa ni nani?

Hawa ni wa kupiga Chini tarehe 28 mwezi huu.
 
Ni moja kati ya kuimarisha sekta ya afya imesaidia sana
Tunachohitaji Watanzania ni bima ya afya kwa watu wote na si maduka ya madawa! Watanzania si wote wataalam wa madawa hivyo wanahitaji madaktari kuwasimamia na kuwaelekeza dawa sahihi kwa maradhi yao!
 
Nenda kakate mbona watu tunazo au unataka ukatiwe
Tunachohitaji Watanzania ni bima ya afya kwa watu wote na si maduka ya madawa! Watanzania si wote wataalam wa madawa hivyo wanahitaji madaktari kuwasimamia na kuwaelekeza dawa sahihi kwa maradhi yao!
 
Ni jambo JEMA kuwa na maduka ya dawa hospitali unayotibiwa, ikiwa tu aina zote za dawa zitapatikana hapo na pili ziuzwe kwa discounted price kama tulipewa na donor country kwasababu hatukuuziwa, serikali inajaribu kurejesha overhead costs ambayo siyo kubwa.

dUKA LA Dawa kuwepo hospitali hata kama limeingia mkataba na serikali kuuza dawa ni jambo jema, ikiwa watazingatia swala la bei, yani bei iwe halali kulingana na gharama zote za dawa tangu manunuzi, usafirishaji, storage na other overhead costs included.

Hakuna dawa ya bure, na bima zielimishwe gharama za dawa na vifaa tiba kwa ujumla ili zinapo charge premium kila mwezi wajue inawatosha , ili mlipaji wa bima naye akifika hospitali afurahie tiba, yani asianze kuambiwa mara ohoo bima yako ndogo, mara dawa hakuna ,mara bima haikulipii hiki na kile.

Mnufaika wa bima aambiwe kabisa kwa kila visit utatakiwa kulipia kiasi Fulani upfront au kwa kila visit bima tutalipia 80% ya gharama zitakazokuja na 20% ya gharama utalipia, ili mnufaika aelewe bima ina cover % ngapi na yake ni % kiasi gani.

Siyo kila kitu kibaya nadhani kuwa na maduka ya dawa hospitali ni sehemu sahihi kuliko haya maduka yakawa huku uraiani bila sababu ya msingi.

Wagonjwa wako hospitali hivyo nadhani ni sahihi maduka ya dawa yakawa hospitalini tu, au basi na kwenye maduka makubwa kama Malls kwa miji mikubwa, na huko mikoani wapange utaratibu mzuri kuliko ilivyo sasa maduka yamezagaa, kama vibanda vya vinyozi.

Dawa laziama ziuzwe ila tunaomba unafuu kama tulisaidiwa na donor country kuzinunua, kama chanjo na baadhi ya vifaa tiba ambavyo tunasaidiwa, na pia serikali ina subsidize kwa kulipia storage na usafirishaji. Kwasababu sisi ndio walipa kodi, basi tupewe discount ya bei kwenye aina hii ya dawa. Ila kwa zile tunazonunua moja kwa moja kwa wakala au mtengenezaji lazima tukubali kulipia full price, hakuna vya bure.

Dawa kama bidhaa nyingine yoyote ina tengenezwa na kuna gharama ziko INVOLVED, kama raw material cost, manufacturing costs, shipping costs na kadhalika, hakuna atakayetugawia dawa bure, unless tuwe tumepewa bure au tumesaidiwa na donors wetu, lakini nazo zina overhead costs tunazopaswa kuzilipia au kama donor alituletea hadi hospitali, hapa tunahaki kuzidai bure kabisa.

Tujielimishe ili tusiwe walalamishi kwa kila jambo.
 
Yaani sijajua how come Serikali inaanza kuuza dawa yaani inafungua maduka ya kuuza dawa.

Badala wajikite kuweka mifumo bora ya afya ikiwemo Bima wao wanakimbilia kuanzisha maduka ya kuuza dawa.

Dawa zinanunuliwa kwa kodi then zinarudi kuuzwa tena, cha kushangaza hospitali na vituo vya afya unakuta kuna panadol pekee.

Aliyetoa wazo la Serikali kuwa na maduka ya madawa ni nani?

Hawa ni wa kupiga Chini tarehe 28 mwezi huu.
😆😆😆😆
 
Hivi kwa mfano serikali inkiweka mfumo wa kila mwananchi kuchangia tsh elf 20 tu kwa mwaka kwenye bima ya afya inaweza kukusanya zaidi ya bilioni 500 kutoka kwa watanzania zaidi ya milioni 50 kwa mwaka. Hii pesa iende kwenye mfuko wa Bima na serikali isiiguze kwa matumizi mengine, hii ishu ya kufungua shops ni kupoteza muda na rasilimali tu.
 
Ni jambo kuwa na maduka ya dawa hospitali unayotibiwa, ikiwa tu aina zote za dawa zitapatikana hapo na pili ziuzwe kwa discounted price kama tulipewa na donor country kwasababu hatukuuziwa, serikali inajaribu kurejesha overhead costs ambayo siyo kubwa...
Lengo la Magufuli kuanzisha maduka mapya ya dawa nje ya Hospitali za umma ilikuwa kuwakomoa wenye maduka binafsi nje ya hospitali hizo , ukimsikia alipokuwa anatia nia hiyo utanielewa, maana aliropoka hadharani.

Kumbuka kwamba kila wodi ya wagonjwa inalo duka la dawa ndani yake, wagonjwa wote kabla ya Magufuli kuingia walinunua dawa kwenye maduka yale, ikiwa kama wakikosa dawa ndio walinunua nje kwenye maduka binafsi, wala hakukuwa na sababu yoyote hata ya kijinga kufungua maduka yaliyoitwa ya MSD nje ya hospitali za rufaa, ilitakiwa dawa nyingi ziwekwe kwenye maduka ya kila wodi ili kuimarisha huduma, kumbuka wodi zile zina wafamasia werevu sana na wazoefu mno.

Haya ndio madhara ya mtu mmoja kudhani ana akili kuliko wote.
 
Lengo la Magufuli kuanzisha maduka mapya ya dawa nje ya Hospitali za umma ilikuwa kuwakomoa wenye maduka binafsi nje ya hospitali hizo , ukimsikia alipokuwa anatia nia hiyo utanielewa, maana aliropoka hadharani...
Naamini kila hospitali hapa nchini ina structure tofauti, au miundombinu kimajengo yako tofauti sana. Ukiongelea muhimbili naweza kukubali kwamba kila wodi labda iwe na pharmacy yake, kwasababu haya majengo ni makubwa sana, Sewa haji, Mwaisela, Kibasila, Out patient clinic, Wodi ya watoto huku, wodi za wazazi kule,psychiatry huku, na MOI na kadhalika ni eneo kubwa na kila jengo linahitaji kujitegemea kama tunaweza.

Ingawa zamani sana, nakumbuka Muhimbili ilikuwa na Pharmacy hapo jingo la Out-patient ili serve purposes vizuri tu, MOI najua wanayo yao, huku JK heart institute wanayo yao. Binafsi naona kama Muhimbili inawezekana, lakini hizi hospitali zingine zinaweza kuwa na Pharmacy mbili moja kwa wagonjwa wa nje na nyingine kwa wagonjwa waliolazwa tu.

Mfumo ulitakiwa uwe hivi, mgonjwa akiingia amuone daktari, apate vipimo, arudi kwa daktari kisha aandikiwe dawa, aende pharmacy apewe hapo hapo hospitali, na kama analazwa basi dawa apewe kwa utaratibu wa kitabibu na madaktari husika kwa usaidizi wa ma-nurse.

Sio mgonjwa kalazwa mnaambiwa mkanunue dawa nje, sasa wamemlaza ili iweje?

Na wagonjwa wa nje kutembea na prescription barabarani wengi huuziwa dawa zisizo kwa kutokujua na hawa wenye maduka baridi huko barabarani.

Hili ni tatizo kubwa na sugu. Lakini akiuziwa pharmacy ndani ya hospitali sio rahisi kuuziwa dawa fake, na kama dawa aliyoandikiwa na daktari haipo, mpharmacia anaweza mwambia mgonjwa nenda kamwambie daktari hiyo dawa aliyokuandikia haipo au haikufai, mwambie akubadilishie iliyopo hapa kwetu ni aina Fulani. Na kwa kufuata taratibu mgonjwa anasaidika na kuapa matibabu sahihi na kupona.

Hii kuzunguka kila kona ya mji unatafuta dawa bei rahisi, unauziwa dawa zisizo kwa bei unayoona inakufaa na unatumia kumbe unajiumiza badala ya kujisaidia.

Kila wodi kuwa na pharmacy kwa hospitali ndogo za wilaya haiwezekani kimfumo na kimuundo, pia sioni kwanini iwe hivyo, ziwepo mbili tu wagonjwa wa nje na moja wagonjwa wa ndani, na kama hospitali siyo kubwa sana wanaweza kushare duka moja hospitali nzima, cha msingi dawa ziwepo.

Nurses wa in-patient hufuata dawa za wagonjwa waliolazwa pharmacy na kuzigawa kulingana na utaratibu na muda aliopangiwa mgonjwa aliyeko chini ya uangalizi.

Hawa wa nje tununue hapo hapo pharmacy na kama hakuna dawa mfamacia atoe taarifa kwenye medical meeting asubuhi au kwa chief medical officer au DMO muda wowote ili naye atoe taarifa kwa madaktari na matatibu waliopo.

Hakuna ubaya wa kuwa na maduka Hospitali mkuu, hapo ndio hasa mahala pake, Bima ni issue nyingine, taaluma ya tiba ni issue nyingine na siasa ni issue nyingine kabisa.
 
Yaani sijajua how come Serikali inaanza kuuza dawa yaani inafungua maduka ya kuuza dawa.

Badala wajikite kuweka mifumo bora ya afya ikiwemo Bima wao wanakimbilia kuanzisha maduka ya kuuza dawa.

Dawa zinanunuliwa kwa kodi then zinarudi kuuzwa tena, cha kushangaza hospitali na vituo vya afya unakuta kuna panadol pekee.

Aliyetoa wazo la Serikali kuwa na maduka ya madawa ni nani?

Hawa ni wa kupiga Chini tarehe 28 mwezi huu.
Tatizo liko wapi. Tujuze
 
Back
Top Bottom