Je, serikali ina nia ya kuboresha kiwango cha elimu, bila kutoa pesa kama inavyoahidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, serikali ina nia ya kuboresha kiwango cha elimu, bila kutoa pesa kama inavyoahidi?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by nickodemus, Mar 28, 2011.

 1. n

  nickodemus Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa makubaliano kati ya Serikali na Benki ya Dunia ambayo inafadhili awamu ya pili ya mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari serikali (SEDP II) iliahidi kufikisha kwenye kila shule ya sekondari nchini Tanzania Tsh 10,000/- kama ruzuku ya kuboresha mazingira ya kusomea ifikipo mwisho wa Januari 2011. Kufikia mwezi Machi 2011 ni asilimia saba (7%) tu ya shule zote za sekondari za serikali Tanzania ndizo zimepata pesa.

  Ufuatiliaji uliofanywa na marafiki wa elimu na wananachi sehemu mbalimbali nchini, na kuratibiwa na HakiElimu, Policy Forum na Twaweza umegundua kuwa asilimia 93 ya shule hazijapata pesa hadi hivi sasa, na zile zilizopata zimepata kati ya Tsh 146/- na 916/- tu kwa mwanafunzi. Kumbuka ahadi ilikuwa ni kupeleka TShs 10,000/- kwa kila mwanafunzi!

  Haijulikani kama hii pesa iliyofika kweli ni ile ya mwaka 2011 ama ni mabaki ya iliyotakiwa kuwa imefika mwaka 2010?

  Kama iliahidiwa Tshs 10,000/- na imeenda Tsh 146/- tu, hizo zingine zimekwenda wapi? Na kama ni za mwaka jana, kwanini zimecheleweshwa?

  Tujiulize je, hizo pesa zingine zitafika lini, je kuna ahadi gani ya kuhakikisha ruzuku kamili ya Tshs 25,0000/- inafika mashuleni kwa wakati?

   
 2. R

  Rangi 2 Senior Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha sana, tena saana.

  Serikali hii ya ccm haina nia ya kuboresha elimu.
  Ni lazima itoke madarakani ifikapo 2015.
   
Loading...