Je, serikali imeshindwa msitu wa hifadhi wa Kagera Nkanda?

Ndege Tausi

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
992
472
Naona uchungu sana kuona jinsi msitu wa hifadhi wa kagerankanda wilayani Kasulu mkoani Kigoma jinsi unavyoendelea kuteketea.

Watu kutoka sehemu mbalimbali na wengine kutoka nje ya nchi wanaendelea kufanya shughuli zao ndani ya msitu huo bila kubugudhiwa.

Kinachoniuma ni jinsi serikali ya mkoa ilivyokaa kimya. Hili tatizo ni la miaka mingi. Naomba ikibidi nguvu kutoka taifani zitumike. Huwa naona wivu sana kuona mikoa mingine kama Kagera jinsi wanavyofanya kazi bila kumuogopa mtu.

Naomba wenye dhamana wahusike na tatizo hili. Labda hawana uchungu kwa kuwa wengi wao hawatoki mkoa huu, sijui?
 
Back
Top Bottom