Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Kama kuna jambo ambalo limekuwa naliona lina mapungufu mengi kisheria ni hili la kutaka watu siyo tu wajiandikishe TCRA wanapofungia 'channels' za YouTube lakini pia kutakiwa kulipa zaidi ya Shilingi milioni moja kila mwaka.
Hii ni kwa sababu mtandao kama YouTube ni bure na Serikali haijawekeza gharama zozote katika uanzishwaji wake wala haina uhusika katika uendeshaji wake. Inapotokea unaweka gharama kama hizi ni kama vile inajinasibisha wewe kama ni mmoja wa wamiliki wake na una mamlaka ya kufanya hivyo kitu ambacho naona wazi kuwa serikali haina mamlaka hayo.
Hii haina tofauti na matapeli wa nyumba na viwanja wanaopeleka watu site wakijidai wao ni wamiliki au mawakala halali wa uuzwaji wa nyumba hizo wakati hata haziuzwi. Hii inalazimisha hata wamiliki wa nyumba kuchafua kuta za nyumba zao kwa maandishi ya 'OGOPA MATAPELI. NYUMBA HII HAIUZWI'.
Juzi nimesikia wameitoza faini YouTube Channel moja kwa kutoweka wazi Terms and Conditions kwa watazamaji wake. Hivi watumiaji wa Youtube wanaweza kujitengenezea terms zao wenyewe tofauti na zile za YouTube ambazo ziko wazi kwa yoyote kuziona? Haya mambo yanachekesha na kustaajabisha sana.
Tushukuru tu kuwa soko letu bado ni dogo sana, hivi hivi Google (wamiliki wa Youtube) wangestahili kuchukua hatua kwenye hili. Au hili jambo linafanyika kwa ushirikiano na Google bila kuwekwa wazi?
Wanasheria wetu mnakwama wapi?