Je, Serikali imedanganya Umma? Wako wapi wenye vyeti feki waliorejeshwa kazini au kulipwa mafao yao?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,599
217,991
Ni vema tukakemea siasa za kishamba na za uongo zinazotaka kuhuishwa nchini mwetu , ikiwa kama kulikuwa na orodha ya wazi kabisa ya wenye vyeti feki Magazetini na kwenye vyombo vingine vya habari nchi nzima, kuna shida gani leo kuorodhesha majina ya wale wanaosemekana walirejeshwa makazini na wale waliolipwa mafao waliyodhulumiwa?

Ni aibu sana uongo mkubwa kama huu kusimamiwa na serikali , tena kupitia kwa Waziri wa Utawala bora , kulikuwa na haja gani ya kudanganya, mbona watanzania walisharidhika na siasa za mwendazake hadi wakamchagua tena kwa karibu 100% kwenye uchaguzi wa 2020?
 
Ni vema tukakemea siasa za kishamba na za uongo zinazotaka kuhuishwa nchini mwetu , ikiwa kama kulikuwa na orodha ya wazi kabisa ya wenye vyeti feki Magazetini na kwenye vyombo vingine...
Pesa ya kuwalipa itatoka wapi? Walisema bei ya mafuta mwezi Disemba itashuka kwa sababu wanaagiza moja kwa moja bila kupitia kwa mawakala, je bei imeshuka? Soma taarifa ya EWURA upate ukweli.
 
Ni vema tukakemea siasa za kishamba na za uongo zinazotaka kuhuishwa nchini mwetu , ikiwa kama kulikuwa na orodha ya wazi kabisa ya wenye vyeti feki Magazetini na kwenye vyombo vingine vya habari nchi nzima...
Serikali haikusema wenye vyeti feki warudishwe kazini kama haujaelewa uliza kilichosemwa ni wale watumishi ambao waliondelewa pamoja na wenye vyeti feki kwa sababu walishindwa kujiendeleza kimasomo kulingana na government order ya mwaka 2004 ilivyoagiza.

Narudia tena wanaorudishwa kazini ni wale walioshindwa kujiendeleza kimasomo na kuondolewa kazini kwa kukosa cheti cha kidato cha NNE .Hakuna mwenye cheti feki atakayerudi kazini, kutumia cheti feki ni kosa la jinai.
 
Mbona kuna watu wameshapokea barua za kurejeshwa kazini..? Na wengine walishafungua mafao wanasubiri tu malipo yao, au hatufatilii wanandugu...?
 
mbona watanzania walisharidhika na siasa za mwendazake hadi wakamchagua tena kwa karibu 100% kwenye uchaguzi wa 2020 ?
Punguza jazba dogo.

Waliorudishwa ni wale darasa la 7 ambao waliachishwa kwa kukosa vyeti stahiki kwa nafasi walizopo,sio mliogushi vyeti,halafu sio lazima wakuambie wewe kama wamerudishwa kazini
 
Ni vema tukakemea siasa za kishamba na za uongo zinazotaka kuhuishwa nchini mwetu , ikiwa kama kulikuwa na orodha ya wazi kabisa ya wenye vyeti feki Magazetini na kwenye vyombo vingine vya habari nchi nzima...
Acha upimbi wewe,vyeti feki hawezi kulipwa mafao wala kurudishwa kazini.

Waliolipwa mafao ni wale la saba ambao hawakuweza kupata sifa za kurejeshwa kazini na waliorejeshwa kazini ni wale la saba waliojiendeleza na kupata cheti cha form 4..

Acha upotoshaji na kukurupuka.
 
Back
Top Bottom