Je, serikali imebadili rasmi tarehe ya malipo ya mishahara na je pensheni inalipwa kama walivyoahidi?

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Kati ya tarehe ambazo watumishi walikuwa nazo uhakika za malipo ya mishahara ni tarehe 23 ya kila mwezi na ikiangukia wkend basi walikuwa wanalipa kabla ya tar hiyo, je kuna kitu gani ambacho hakiko sawa maana hata serikali haija tangaza rasmi tarehe mpya ya malipo ya mishahara kuwa imebadilika hadi muda huu mishahara bado tafsiri yake ni nini.

Pensheni ziliahidiwa kulipwa mapema na kwa muda mchache sana, sasa hivi kaka yangu ni Askari Polisi amestaafu mwezi wa 4 Mwaka huu 2021, nyaraka zote za kustaafu aliziwasilisha Dodoma mwezi 12 mwaka jana 2020. hadi sasa hajapata pensheni yake hii pia maana yake nini kufuatia kauli na ahadi ya Marehemu Magufuli na Rais aliyepo madarakani. Je kuna nini ambacho kina sababisha na hakija kaa sawa.
 
JPM pamoja kulikuwa na ujenzi wa miundo mbinu nchi nzima pamoja na project nying lakini mlilipwa mshahara wenu mapema tena walimu ambao ndio watumishi wengi wa umma kuliko vitengo vingine walikula mshahara wa bure kipindi cha Corona

Sasa hyu mama yenu atawakomesha ...
 
Weee jamaa kila mwez unalalamika kuusu mshahara kama vip njoo ulimwengu wa kupambana uachane na vihela vya mwisho wa mwez
Hakika, Vihela vya mwisho wa mwezi ni shida na kupumbazwa akili.
Ukiviangalia hivyo huendelei kabisa.
Mi kwa siku moja nakunywa pombe ya zaidi ya laki moja. Hiyo ni pombe tu.
Hiyo ni baada ya kutafuta mapato ya ziada.
Mfanyakazi unashindwa kunywa pombe za japo elfu 20 kwa siku, tambua kwamba huishughulishi akili yako.
Umeridhika na mshahala na utakufa masikini.
 
Mwezi wa saba ndio mwaka mpya wa fedha. So kuna kufunga hesabu za mwaka uliopita na kuanzisha accounts za mwaka huu. kwa hiyo ucheleweshaji huu ni wa kawaida kuwa mvumilivu.

Kuhusu huyo ndugu yako polisi natamani asilipwe hata mia. naamini atakuwa amekula za kutosha za walala hoi toka ameanza kazi.
 
Matamko ya wanasiasa majukwaani huishia majukwaani.

Huyo "mwera" atulie Hadi miezi nane ipite ndiyo aanze kuulizia pensheni na atalipwa pungufu.
 
Jpm pamoja kulikuwa na ujenzi wa miundo mbinu nchi nzima pamoja na project nying lakini mlilipwa mshahara wenu mapema tena walimu ambao ndio watumishi wengi wa umma kuliko vitengo vingine walikula mshahara wa bure kipindi cha Corona

Sasa hyu mama yenu atawakomesha ...
"Mshahara wa bure"

Ni upi huo?
 
Hakika, Vihela vya mwisho wa mwezi ni shida na kupumbazwa akili.
Ukiviangalia hivyo huendelei kabisa.
Mi kwa siku moja nakunywa pombe ya zaidi ya laki moja. Hiyo ni pombe tu.
Hiyo ni baada ya kutafuta mapato ya ziada.
Mfanyakazi unashindwa kunywa pombe za japo elfu 20 kwa siku, tambua kwamba huishughulishi akili yako.
Umeridhika na mshahala na utakufa masikini.
Saf kabsa mpambanaji
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom