ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 42,390
- 49,040
Picha: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni
SERIKALI imelieleza Bunge kuwa hairuhusu uraia pacha kwa watu wazima isipokuwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni, alitoa kauli hiyo bungeni jana alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Agnesta Lambert.
Alihoji kama serikali iko tayari kuruhusu uraia pacha kwa Watanzania wenye uraia wa nchi nyingine.
Akijibu swali hilo, Masauni alisema uraia wa Tanzania unaongozwa na Sheria ya Uraia ya Tanzania Sura ya 357, marejeo ya mwaka 2002.
“Sheria hii inabainisha aina tatu za uraia wa Tanzania ambazo ni uraia wa kuzaliwa, uraia wa kurithi na uraia wa tajnisi. Kwa mujibu wa Sheria ya Uraia tajwa hapo juu, serikali hairuhusu uraia pacha kwa watu wazima isipokuwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18 ambao wanakuwa na uraia wa Tanzania na uraia wa nchi nyingine,” alisema.
Source: Nipashe