FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 37,898
- 43,806
Kwa uelewa wangu kodi ni makato ya kipato ulichoingiza. Mfano nimeuza bidhaa kwa sh.100,000/=, ambapo mimi nilinunua kwa bei ya jumla sh.80,000/=, hivyo gross profit yangu ni sh.20,000/=. Nikitoa gharama mbalimbali nabakiwa na net profit ya 10,000/=. Je, natakiwa nilipe 18% ya 10,000/= au ya 100,000/=?