Je, Sera ya Serikali ya majimbo ya CHADEMA ni suluhu ya umasikini katika nchi yetu?

mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
1,042
1,454
Wanabodi niende moja kwa moja kwenye mada, nimekuwa nikifuatilia mikutano ya wagombea wa urais hasa wa chama cha mapinduzi (CCM) na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)

Katika mikutano yao wote wanazungumzia kuondoa umasikini katika nchi yetu na wote wanamkubali kuwa Tanzania ni nchi tajiri sana, lakini watu wake bado ni masikini. Sijamsikia hata mgombea wa CCM akisema sasa watanzania wameondokana na umasikini naye anasema watanzania ni masikini ila nchi ni tajiri sana.

Maswali ambayo watanzania wengi tunajiuliza ni kwanini nchi ambayo ni tajiri sana watu wake wawe masikini sana, jibu la haraka ni kwamba ama kuna watu wachache wanaotumia utajiri wa nchi yetu, au hakuna sera nzuri ya kuwezesha wananchi kujiletea maendeleo yao. Nasema hivo sababu ziko baadhi nchi zina utajiri wa mafuta lakini watu wake ni masikini na mafuta yanauzwa miaka yote sababu ni wachache wananufaika na hayo mafuta.

Mgombea wa CCM na mgombea wa CHADEMA wote wanajaribu kutueleza namna walivyo na sera ya kutuomdoa katika huo umasikini lakini ukisikiliza sana sera za CCM hazioneshi kuwa na tofauti yoyote na sera za miaka iliyopita ambazo zinaongelea kujenga barabara, reli, hospital, shule ,kusambaza,umeme na mengine mengi. Kwa maneno mengine ni namna seriakli inavyoweza kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Ukisikiliza sera ya mgombea wa CHADEMA anazungumzia katiba mpya, kugatua madaraka, uhuru wa watu, haki, utawala wa sheria, kubadilisha mfumo wa kodi, wakulima kuwa uhuru kuuza mazao yao kwa maneno mengine wanazungumzia namna ya kumuwezesha mwananchi kujiletea maendeleo yake badala ya kutegemea serikali

Kuna msemo unasema huwezi kuendelea kufanya mambo kwa utaratibu huo huo na kutegemea matokeo tofauti. Ninasema hivyo kwa kujaribu kuangalia sera ya CCM na kuangalia ina tofauti gani na sera zilizopita ukilinganisha na sera ya CHADEMA na jinsi sera hizo zinavyoweza kusaidia kuwaondoa watanzania katika huu umasikini wakati nchi yetu ina utajiri mkubwa ambao wagombea wote wawili wanakili kuhusu hilo.

Ninaiona sera ya CHADEMA inajikita kutatua tatizo la umasikini wa watanzania kwakuwa inaleta mawazo tofauti kabisa inazungumzia Katibu kwa maana ya kupunguza madaraka ya Rais na kuwapa madaraka makubwa wananchi, na hivyo kuwaaminisha wananchi kuwa maendeleo yao hayawezi kuletwa na seriakali yataletwa na kila mwananchi mmoja mmoja.

Katika sera ya CHADEMA nimevutiwa zaidi na seriakli za majimbo kwakuwa itasaidia kutatua tatizo la kuchezewa kwa rasilimali za nchi kutokana na kwamba wananchi watakuwa na uwezo wa kuwawajibisha moja kwa moja viongozi wao ambao watakuwa wakuchaguliwa na wananchi.

Katika mfumo wa utawala wa majimbo hakutakuwa tena na haja ya kusubiria viongozi wakuu kutembelea maeneo yetu na kubaini ubadhirifu unavofanywa na wateule wao ambao bila viongozi wakubwa kuubaini wananchi hawana uwezo wa kusema chochote kwa mfumo wa utawala uliopo.

Kwa muundo wa seriakali ulivyo kwa sasa ni vigumu sana mtu mmoja kuwa na maamuzi ya nchi kubwa kama Tanzania na kujuwa vipaumbele vya kila maeneo badala yake yeye anakuwa na vipaumbele vyake na siyo vipaumbele vinavyotokana na shida za wananchi katika maeneo yao mbali mbali.

Binafsi sidhani kwamba kweli watanzania tutaweza kutatua tatizo la umasikini ujinga na maradhi kwa kuendelea na hizi sera za kutegemea serikali kuu kujenga madaraja, barabara, shule mahospital ambavyo tangu tupate uhuru tumekuwa tunajenga na watanzania bado wanakabiliwa na tatizo la umasikini, ujinga na maradhi hadi leo.

Ninakubaliana na sera za CHADEMA kuwa tunahitaji mabadiliko ya katiba yetu, tunahitaji mabadiliko ya muundo wa serikali, kuimarisha sekta binafsi, uhuru wa vyombo vya habari uhuru wa wananchi kutoa maoni yao, utawala wa sheria na mengine mengi ili yote hayo yasaidie mtanzania mmoja mmoja kujiletea maendeleo yake kutokana na kuwa huru katika kufanya shuguli zake za kiuchumi.

Hapa tunahitaji business unusual ili tuweze kutoka katika huu umasikini wa wananchi wetu.

Naomba kutoa hoja.
 
Back
Top Bottom