Je Sasa Ni Rasmi JK kamtosa Membe? Tusubiri A Surprise Candidate wa CCM?

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,531
8,616
Mwenendo wa kuelekea mwaka 2015 unaanza kujionesha ...Historia ya Nchi Hii imeonyesha wazi kuwa hakuna Rais aliyeweza Kuweka Rais amtakaye akiwa madarakani ...ni Jambo la kujivunia hili....Mwalimu alishindwa ataweza nani ??
Mwalimu alimtaka Sokoine amridhi ( akafariki) akamtaka Salim ( wahafidhina wakamzunguka ..hata Baada ya kuwa amempanga Mwinyi kukataa uteuzi)
Mwinyi ...hakufanikiwa kuweka Rais aliyemtaka mwaka 1995....na safari Hiyo aliyekuwa na karata ni Mwalimu.......hata Mkapa ikibidi afanye u turn mwisho kukubali Kikwete ....hasa kwenye ile hotuba yake ....aliposema.." Sasa ni Zamu ya rika jipya..." Ni wazi alikuwa anaonyesha kuelekeza nani apite...

Kikwete ambaye anaeleweka ni bingwa wa Siasa Za mikakati .....anaelekea hataki kufanya makosa ya watangulizi wake...ni wazi kwa namna Fulani Sasa anajitenga na marafiki zake ...wa mtandao....Alianza kumweka Mbali Lowassa...jambo ambalo ..Membe lilionekana kumpa Nguvu kubwa na kujiendelea kuwa karibu na familia Kuu akifikiri wameshika ticket.......mwelekeo wa Mwezi mmoja uliopita ...UKianza..
1 . Kumkana Membe na Kauli zake Za EAC na coalition of the willing ...na kutoa Kauli mpya iliyoonesha kuwa Membe ni waziri anayetoaa misimamo ya Nchi bila kufikiri,kushirikisha ...Rais au baraza...ilikuwa pia aibu mkizingatia Kauli Za hapo nyuma Juu ya Malawi
2. Jana pale uwanjani aliongelea ...onyo kwa mtu yeyote anayegombea kwa nia ya kulipizaa kisasa ( ni wazi mgombea aliyetoa Kauli ya Kisasi ni Membe peke yake ......aliposema anao " MAADII KUMI NA MOJA" ambao waombe asioteshwe( urais) ..watahama Nchi...

Maneno yote haya yapo na yalinakiliwa na vyombo Vya habari tv ,magazeti na mitandao....

NI WAZI KUWA SASA RAIS ATAMPA UGOMBEA RAIS ATAKAYEPITISHWA NA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPUNDUZI......WANAOGOMBEA KWA KUTEGEMEA KUJIPENDEKEZA KWA RAIS ..MKEWE AU FAMILIA KWA UJUMLA LWA KIGEZO CHOCHOTE WAJUWE SASA KIKWETE HANA UWEZO WA KUTOA MGOMBEA...KAMA AMBAVYO WAGOMBEA WALIOPIGIWA CHAPIO NA MARAIS WOTE WALIOTANGULIA WALIKATALIWA...NA HATA SASA ...KUWA KARIBU NA RAIS HAITAKIWA SIFA BALI NI DISQUALIFICATION....
WAGOMBEA AMBAO WAMESHAGUNDUA KUWA RAIS HANA FUNGUO NA WANAJIWEKA NA WANANCHI AU WANACHAMA....NDIO WATAKAOKUWA NA NAFASI KUBWA ..NAONA KAMA WATATU HIVI ..HADI SASA....UKITOA HUYO MMOJA AMBAYE AMEKUWA KWENYE KWAPA LA FIRST FAMILY....

HONGERA KIWETE KWA KUGUNDUA MAPEMA KUWA HUTAWEZA KUMWEKA RAIS ...UMEJIWEKA HURU.... Na hongera kwa kutoa onyo dhidi ya kisasi ..hili hata Nyerere akiwaonya wazambia..hawakusikia Leo Hii kila Rais anayestaafu Huko lazima afungwe na mrithi wake ...Sasa hivi Rupiah Banda kampokea Marehemu Chiluba ufungwa .......
 
Mnahangaika bure Rais wa Tanzania 2015 ni Amani Abeid Karume


Karume huyu huyu maCCM mliemzomea kule Chimwaga hadi akawaambia mna akili kama za samaki??!!

Kikwete kuepusha purukushani na kufirigisana ndani ya chama itabidi ampigie chapuo Migiro kwani anataka pia mtu ataemlinda kwa hali na Mali kwa madudu yake atakapostaafu!!
 
Bavicha bana wao wanajina wanahaki kuisemea CCM
Kinyume chake utaandamwa ooh fuatilia yako
Hebu malizaneni kwanza na Zito na Kitila
 
Mnajisumbua bure the suprise candidate wa CCM 2015 ni Stephen Wassira. Hizi taarifa nyeti.
tunahitaji sana rais mwenye sura ngumu, labda atasaidia kutisha wachina maana wamezidi:shocked::shocked:
 
Karume huyu huyu maCCM mliemzomea kule Chimwaga hadi akawaambia mna akili kama za samaki??!!

Kikwete kuepusha purukushani na kufirigisana ndani ya chama itabidi ampigie chapuo Migiro kwani anataka pia mtu ataemlinda kwa hali na Mali kwa madudu yake atakapostaafu!!

Rais MWANAMKE Tanzania at least bado for now...Hii nafasi ya Spika...ni nafasi kubwa mno kushkwa na MWANAMKE ..tutaifanyia kwanza Tathmini..kuamua Kama tuwape Nchi...tutaangaliaa uongozi wa Joyce Banda..na Hellen Sirleef ..na utamaduni wetu hasa mfumo dume...namna ya kuutokkomeza...kabla ya kuamua..pia tutaangalia

Kimataifa tumukuwa na asha rose migiro na Getrude Mongella ...tutaangalia uendaji wao....pia tutaangalia Kama wanawake wapo tayari kuwaamini wenzao
 
Jamani hili jambo sio la kuletea mchezo.Ushaabiki wa kanda,dini,kabila,urafiki n.k. hauitajiki.Tunahitaji rais atakae jenga uchumi na kuliweka jungu kuu(hazina) katika hali nzuri.Watumishi wenzangu serikalini wataniunga mkono jinsi hali ilivyo mbaya maofisini.Mambo mengi yamesimama kwa sababu pesa hakuna.Zimebaki siasa majukwaani tu.
 
Bavicha bana wao wanajina wanahaki kuisemea CCM
Kinyume chake utaandamwa ooh fuatilia yako
Hebu malizaneni kwanza na Zito na Kitila

Nadhani siku ikiisha bila kutaja neno lolote linaloihusisha CHADEMA (hata pasipostahili) utakufa!
 
Tulitegemea labda Waziri mkuu Pinda angeleta ushindani mkubwa wa kuamua nani awe rais wa Tanzania. Lakini matarajio ya wachache yamekwisha kwa lumumba. Waliochanganyikiwa ndani lumumba ambao matumaini yao yalikuwa kwa fisadi lowasa wamekosa matumaini kabisa maana walikuwa wamesahau kuwa rais wa Tanzania hajawahi kutoka kwenye kundi la watanzania wa kawaida (mf mkulima, mfugaji nk) kama alivyo lowasa ni mfugaji fisadi.

Nafikiri ni busara walau rais akamtimua kazi Pinda na amweke waziri mkuu ambaye baadaye 2015 ataleta changamoto kwa CDM. CDM wanataka mgombea ambaye ataleta changamoto kipindi cha uchaguzi ujao. Maana kwa CDM mapambano ni hadi kieleweke. Na urais ni kwa CDM taka usitake.

Hivyo ninamsihi mhe Rais Kikwete amteue waziri mkuu imara ndani ya Baraza lake la mawaziri au miongoni mwa Wabunge wake ambaye walau atasimamia utendaji serikalini. Wapo wachache ambao walau wana uwezo wakipewa nafasi.

Mfano: Dr. Harrison Mwakyembe. Hatumfahamu vizuri lakini anauwezo mkubwa sana wa kuwa Waziri mkuu na hata kuwa rais.
au Dr John P. Magufuli. Huyu nafasi ya uwaziri mkuu anaimudu sana tatizo kwake ni urais hawezi. Si mbaya sana hata kwa nafasi hiyo tu.

Tunaamini Rais atatumia busara kuliko kuacha nchi kwa manyang'awu kama lowasa wanaohonga na kurubuni kila mara mtaani, makanisani na misikitini. Hila za namna hii ni ya hatari sana kwa mstakabali wa nchi yetu. Kutafuta urais kwa gharama yoyote ni jambo la hatari kweli. Mungu tuepushe na laana hii.
 
Back
Top Bottom