Je Sasa Ni Rasmi JK kamtosa Membe? Tusubiri A Surprise Candidate wa CCM?

tusubiri wakati ufike halafu ndiyo tuamue kwa sasa mda bado sana tunapoteza mada.
 
JK anasema watu wasilipize kisasi.Hii ni defensive mechanism
vipi na wewe unaoteshwaga na kalumanzila????!!!!!
he don't have to defend himself from anyone, the next president will come from the party he is chairing. and more than 2/3 of the mp's will come from the same. why should he be afraid??
leta tafsiri zako za kichaga
 
Matumizi ya herufi kubwa na ndogo katika post hii yanakaribisha fikra kwamba mwandishi alishachoshwa na umande katika jitihada zake za awali za kufuta ujinga.

Kadhalika kichwa cha habari kinauliza swali lakini habari aliyoiandika haina swali na badala yake inampongeza JK. Shule shule shule!!

SASA MNAKUWA WALIMU WA mwandiko ...BADALA YA KUJADILI HOJA ILIYO MEZANI...??? RAIS AMEONGELEA WANAOTAKA URAIS WA KULIPIZA KISASI...AMENAKILIWA NA VYOMBO VYA HABARI PIA ..SIO HABARI YA KUBUNI HII.....SASA INAKUWAJE WATU WANAJIKITA KWENYE KUSAHIHISHA MWANDIKO MARA LITERATURE ..SIJUI NINI .......
LETS BE SERIOUS ! SIO LAZIMA WOTE TUWE VIONGOZI ..INATOSHA KUWA RAIA WA KAWAIDA TENA WAPIGA KURA !....MAANA SASA KAZI HAZIFANYIKI KISA URAIS ALAAAAA....BASI WANAOUTAKA WAJIUZULU KWENYE UTUMISHI WA UMMA WAFANYE KAMPENI....NA WAACHE KUTISHA WENZAO....KISASI HATUTAKI!!!
 
aaaaah sihasa (siasa),
mimi nafikili 2015 inabidi watz wote tufe nchi ianze upya (yaani kije kizazi kipya).
au tuombe mungu awafufue hawa watuongoze.

adolph hitller - raisi wa tz , mkuu wa majeshi.
idd amin - waziri mkuu,
muamall gaddafi - makamu wa raisi, waziri wa ujenzi na uchukuzi.
saddam hussein - waziri wa nishati, maliasili,
osama bin laden - waziri wa fedha.

onyo; hizo wizara zinatosha.
bunge litakuwa hakuna ila wakuu wamikoa watakuwepo, wanatakiwa walipoti kwa waziri mkuu na ndio atawateua.
kila mkuu wa mkoa atawajibiki kwa kila uzembe wa mkoa wake.

hivi ni marufuku - wizara ya michezo (bado mda wa kucheza).
wabunge (kazi kwanza, commeddy baadaye)
 
Mwenendo wa kuelekea mwaka 2015 unaanza kujionesha ...Historia ya Nchi Hii imeonyesha wazi kuwa hakuna Rais aliyeweza Kuweka Rais amtakaye akiwa madarakani ...ni Jambo la kujivunia hili....Mwalimu alishindwa ataweza nani ??
Mwalimu alimtaka Sokoine amridhi ( akafariki) akamtaka Salim ( wahafidhina wakamzunguka ..hata Baada ya kuwa amempanga Mwinyi kukataa uteuzi)
Mwinyi ...hakufanikiwa kuweka Rais aliyemtaka mwaka 1995....na safari Hiyo aliyekuwa na karata ni Mwalimu.......hata Mkapa ikibidi afanye u turn mwisho kukubali Kikwete ....hasa kwenye ile hotuba yake ....aliposema.." Sasa ni Zamu ya rika jipya..." Ni wazi alikuwa anaonyesha kuelekeza nani apite...

Kikwete ambaye anaeleweka ni bingwa wa Siasa Za mikakati .....anaelekea hataki kufanya makosa ya watangulizi wake...ni wazi kwa namna Fulani Sasa anajitenga na marafiki zake ...wa mtandao....Alianza kumweka Mbali Lowassa...jambo ambalo ..Membe lilionekana kumpa Nguvu kubwa na kujiendelea kuwa karibu na familia Kuu akifikiri wameshika ticket.......mwelekeo wa Mwezi mmoja uliopita ...UKianza..
1 . Kumkana Membe na Kauli zake Za EAC na coalition of the willing ...na kutoa Kauli mpya iliyoonesha kuwa Membe ni waziri anayetoaa misimamo ya Nchi bila kufikiri,kushirikisha ...Rais au baraza...ilikuwa pia aibu mkizingatia Kauli Za hapo nyuma Juu ya Malawi
2. Jana pale uwanjani aliongelea ...onyo kwa mtu yeyote anayegombea kwa nia ya kulipizaa kisasa ( ni wazi mgombea aliyetoa Kauli ya Kisasi ni Membe peke yake ......aliposema anao " MAADII KUMI NA MOJA" ambao waombe asioteshwe( urais) ..watahama Nchi...

Maneno yote haya yapo na yalinakiliwa na vyombo Vya habari tv ,magazeti na mitandao....

NI WAZI KUWA SASA RAIS ATAMPA UGOMBEA RAIS ATAKAYEPITISHWA NA WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPUNDUZI......WANAOGOMBEA KWA KUTEGEMEA KUJIPENDEKEZA KWA RAIS ..MKEWE AU FAMILIA KWA UJUMLA LWA KIGEZO CHOCHOTE WAJUWE SASA KIKWETE HANA UWEZO WA KUTOA MGOMBEA...KAMA AMBAVYO WAGOMBEA WALIOPIGIWA CHAPIO NA MARAIS WOTE WALIOTANGULIA WALIKATALIWA...NA HATA SASA ...KUWA KARIBU NA RAIS HAITAKIWA SIFA BALI NI DISQUALIFICATION....
WAGOMBEA AMBAO WAMESHAGUNDUA KUWA RAIS HANA FUNGUO NA WANAJIWEKA NA WANANCHI AU WANACHAMA....NDIO WATAKAOKUWA NA NAFASI KUBWA ..NAONA KAMA WATATU HIVI ..HADI SASA....UKITOA HUYO MMOJA AMBAYE AMEKUWA KWENYE KWAPA LA FIRST FAMILY....

HONGERA KIWETE KWA KUGUNDUA MAPEMA KUWA HUTAWEZA KUMWEKA RAIS ...UMEJIWEKA HURU.... Na hongera kwa kutoa onyo dhidi ya kisasi ..hili hata Nyerere akiwaonya wazambia..hawakusikia Leo Hii kila Rais anayestaafu Huko lazima afungwe na mrithi wake ...Sasa hivi Rupiah Banda kampokea Marehemu Chiluba ufungwa .......

Sera za udini walizoanzisha zitawamaliza...

Watajitahidi kujikita mule mule ku-maximize chance...
 
Mpende msipende Rais wa Tanzania 2015 ni Zitto Kabwe kupitia Ccm.
Kwa sasa ndie anaepigiwa debe sana na wana Ccm ktk mitandao yote ya kijamii.

Hata baada ya kuvuliwa madaraka yote ndani ya chama chake cha CHADEMA, wana Ccm wengi hawakufurahishwa na hatua hiyo ndio maana wanajitahidi kuhujumu mikutano ya katibu mkuu wa Chadema Mkoani Kigoma.

Zitto ndie pekee hana makundi ndani ya CCM,na ndie mtu pekee ambae anakubalika hata na mwenyekiti wa Ccm hata kutaka kumuoza binti yake.
 
vipi na wewe unaoteshwaga na kalumanzila????!!!!!
he don't have to defend himself from anyone, the next president will come from the party he is chairing. and more than 2/3 of the mp's will come from the same. why should he be afraid??
leta tafsiri zako za kichaga

Pathetic indeed....!
 
Jamani hili jambo sio la kuletea mchezo.Ushaabiki wa kanda,dini,kabila,urafiki n.k. hauitajiki.Tunahitaji rais atakae jenga uchumi na kuliweka jungu kuu(hazina) katika hali nzuri.Watumishi wenzangu serikalini wataniunga mkono jinsi hali ilivyo mbaya maofisini.Mambo mengi yamesimama kwa sababu pesa hakuna.Zimebaki siasa majukwaani tu.
Pesa zipo ila umekosa pesa za michongo ndo maana unapiga kelele.

 
Mpende msipende Rais wa Tanzania 2015 ni Zitto Kabwe kupitia Ccm.
Kwa sasa ndie anaepigiwa debe sana na wana Ccm ktk mitandao yote ya kijamii.

Hata baada ya kuvuliwa madaraka yote ndani ya chama chake cha CHADEMA, wana Ccm wengi hawakufurahishwa na hatua hiyo ndio maana wanajitahidi kuhujumu mikutano ya katibu mkuu wa Chadema Mkoani Kigoma.

Zitto ndie pekee hana makundi ndani ya CCM,na ndie mtu pekee ambae anakubalika hata na mwenyekiti wa Ccm hata kutaka kumuoza binti yake.

Hivi Kweli ...are you serious...hata Kama anahamia Huko ........ CCM ni wahafidhina kwa ASILI ...hawawezi Kumpa cheo mtu ambaye Hana roots....labda Ubunge na uwaziri...
 
Hapana; maana ya kisasi ambacho kikwete anatahadharisha ni yale ya kutaka walio jilimbikizia mali kuulizwa walizipataje, na kulazimiswa wazirudishe. Walio iba na kufisadi kuhukumiwa. Mali zilizochangiwa na watanzania wote na CCM ikazimiliki peke yake tu, kutaka izirudishe serikalini. Nyumba zilizokwapuliwa serikalini kutakiwa kurudishwa. Mali za umma kama viwanda, mahoteli, nk virudi mahali pake. JK yeye alikuwa anaisihi serikali ijayo ifanye maridhiano kwa hayo juu, kama Mandela alivyo fanya huko Afrika Kusini.
 
Mheshimiwa Rais Kikwete anatuongoza watu ambao hatutaaki hata kufuatilia mwenendo wake, matendo yake na kauli zake!!!!

Kuondolewa kwa Lowassa ilikuwa agenda ya watu wanaosumbuliwa na rekodi tukuka za Taasisi ya Urais....walio mashabiki wa kupima viongozi wetu kwa dini zao walijipanga mapema via Six(bila yeye kujua ilhali hamu ni kisasi cha kunyimwa u PM), JK knew with Lowassa as Premier atafanikisha njozi zake kama mkuu wa nchi lakini wapi makajanja yakaanza kumpaisha Lowassa through media though he deserved those praising but makanjanja walijipanga kutumia hilo kama turning point.....wakafanikiwa.

Rais alimwacha Kamanda wake akasulubiwa na kudhihakiwa lakini baadae ameuona mchezo wa Makanjanja ulilenga wapi.... ndipo akatamka

"Tuache kujeruhiana na kuchafuana eti kwa sababu ya kupata tikiti ya kugombea u Rais 2015, tusipoangalia tutapata Mgombea ambaye yuko na bandeji kila sehemu ya maungo yake na tukataabika kumuuzakwa Wananchi"

Huyu ni Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete. Kwanini hapa Jf Mod usijaribu kutupatia majumuisho ya Mkuu ktk ilani zake juu ya wapendao Urais......ili tujitafakari pamoja naye.
 
Kwa siasa za sasa hv migiro hawez himili vishindo,na pia kumlinda jk ni ngumu kwa kuwa jk ana tuhuma.nyingi.za ufisadi yeye na mwanae ritz
 
Back
Top Bottom