Je sare za shule kwa wanafunzi S/Msingi na S/Sekondari ziondolewe?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,339
38,982
Kutakuwa na faida au hasara gani endapo wanafunzi hasa wa shule za msingi na sekondari kuondolewa kuvaa sare kwenye shule za umma?
 

Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,540
13,439
Hasara ni kwamba watoto waweza toroka shule bila mwalimu hata wanajamii wengine kuwashtukia!

Pia watoto wengine wataenda matak0 nje kwa kuwa wazazi wengine licha ya uwezo kuwa mdogo hawataona umuhimu wa kununua nguo "mpya" kwa ajili ya shule

Gap ya watoto toka familia za kipato cha juu na cha chini zitakuwa obvious

Mwisho uniform zinapendeza angalia wajeshi; maaskari; scout hata cheer groups kwenye mashule ya wasiovaa uniform au siku ya graduations.
 

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,631
8,445
Swali juu ya swali, Marekani kwenye public schools hawavai yunifomu. To be more specific to your question the answer is "Italy"
Good one Mkuu

Ila MMM hajasema kabisa ni wapi swali lake linakava.... and i still believe kuna room ya someone to take a mickey out of the question (pemba?, Unguja? Mafia? the whole country?, Tanganyika??)

Anyway back to topic

Hasara ni kubwa sana kijamii zaidi hasa ukizingatia uniform could be the only good dress to some kids, pia psychologically inawaletea watoto usawa na it is easy to track kids kwa shule wasomazo

...others are providing different markers (e.g. weruweru walikua na color specific kwa darasa, jitegemee wana "nyota" nk) na inasaidia zaidi any form of tracking kwa kids

I wouldnt like kuodnoa uniform kwa sababu za kijamii tu......... what if wengine wakija na vibukta, wengine xxxx nk
 

Likwanda

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
3,914
1,115
Kuvaa Unifoam Kunawawezesha Waalimu Kuwatambua Wanafunzi Wao Kwa Urahisi Zaidi, Hivyo wanakua na full control ya wanafunzi wanapokuwa hapo shuleni.
 

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,690
625
Kwani kwa miaka yote hiyo wanafunzi wamekuwa wakivaa sare, kuna mapungufu gani yamejitokeza?

Tulianza kuiga vichupi, vitop, na milegezo, hiyo haijatosha hadi leo hii tena mnataka wototo wetu wasivae`uniform.
Tunataka kujenga jamii gani hiyo?

Kuna kero nyingi tu zinazoikabili jamii yetu, ni vema kuzijadili na pengine kuzipatia utatuzi hapa badala ya kutumia muda wetu kujadili vitu ambavyo kwa mtazamo wangu havina ulazima wa kupata air time hapa.

Let's be serious jamani.
 

TAMKO

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,090
762
Natoa Tamko: Tuanze na mada A.. Fimbo.. kisha maada B.. uniform..
 

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
204
Mie naona huko tuendako zitafutwa kwani hata sasa zinasuasua. Zamani zetu uniform zilikuwa uniform na sasa hata ukivaa kama ninja ruksa
 

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,902
3,079
Vijana wa siku hizi...suruali za shule wanashona 'vimodo' na madem 'vimini'...sipati picha sare za shule zikifutwa. Maana sasa hivi zipo lakini watu wanavaa ajabu ajabu, je zikiondolewa sare za shule.

Zamani wanawake kupaka nywele dawa ilikuwa inakatazwa, sasa hivi kuna shule zinaruhusu. Taaaaratibu taratibu mambo yanabadilika.

Kusema ukweli mimi nilikuwa sipendi uniform, bora hata chuoni hakuna kitu kama hiyo. Uniform zinaboa sometime. Ila cha msingi ni wanafunzi kujitambua. Ukijitambua hata usipovaa uniform au ukivaa uniform utaonekana smart.
 

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
13,631
23,368
Kutakuwa na faida au hasara gani endapo wanafunzi hasa wa shule za msingi na sekondari kuondolewa kuvaa sare kwenye shule za umma?

Katika nchi yetu hii iliyojaa choyo na ubinafsi kama uniform zitaondolewa baada ya muda mfupi utaona mashindano ya mavazi shuleni baina ya watoto wenye kutoka katika familia zenye ahueni ya maisha na wale wa kutoka familia duni. Kwa jinsi watoto wasivyoweza kuvumilia mwenzake anapokuja na viwalo vipya basi nachelea kusema baadhi wataadhiriwa sana kwenye perfomance darasani. Nadhani tuache uniform ziendelee kuvaliwa kwa primary na Secondary. Kwa wale wa collage na university tuwaache waendelee kushindana kuvaa vitop MMK
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Umuhimu wa sare Tanzania:
1. Inaleta usawa.
Wazazi wengi wa kitanzania ni wavivu kuwanunulia watoto wao nguo, pia kutokana na vipato kuwa tofauti, itawafanya wale wenye kipato cha juu kuwanunulia watoto wao nguo za bei ya juu, itaongeza matabaka.

2. Zinapendezesha shule.
Sare za shule zinapendezesha shule sana.

3. Utambulisho.
Sare zinatumika ktk kumtambulisha mwanafunzi ktk jamii.

NB. Point ya kwanza ni muhimu zaidi kwangu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom