SoC01 Je, Sarafu za Kimtandao (cryptocurrencies) ni fursa nyingine kwa Vijana wa Kitanzania?

Stories of Change - 2021 Competition

chief lobengula

New Member
Jul 17, 2021
3
15
Habari zenu wanajukwaa. Natumaini ni wazima wa afya. Namshukuru Mungu kwa uzima aliotupa siku ya leo.

Mnamo Juni, 13 2021, Rais wa JMT Mh. Samia Suluhu Hassan alitoa wito kwa Benki Kuu (BOT), kujiandaa kwa ajili ya kulipokea swala la sarafu za kimtandao na teknolojia inayoziwezesha yaani blockchain technology.

Leo tuangalie upana wa fursa hii kwa watanzania. Kwanza kabisa.

Sarafu ya kimtandao ni nini?

Ni sarafu ambayo haishikiki kwa mkono (virtual), ambayo hairatibiwi au kuongozwa na mamlaka au serikali. Kwa lugha rahisi ipo decentralized.

Sarafu ya kimtandao ya kwanza kuanzishwa ilikuwa ni Bitcoin ambayo ndio sarafu maarufu na yenye thamani kuliko zote. Ilianzishwa mwaka 2009 ikiwa na price ya Dola za kimarekani zero.

Muamala wa kwanza kufanyika kwa kutumia Bitcoin ulifanyika tarehe 22 Mei 2010, ambapo Mmarekani mmoja mkaazi wa Florida aitwae, Laszlo Hanyecz alitumia Bitcoin 10, 000/= zilizokuwa na thamani ya dola za kimarekani 25 tu (10,000=25) kununua pizza mbili.

Baada ya hapo bei ya Bitcoin moja ikaanza kupanda kutoka 0.46USD mwezi Desemba 2010 hadi sasa wakati naandika mnakasha huu bei yake ilikuwa 33816USD.

Sarafu hizi zinakuwezesha mtumiaji kufanya muamala bila ya kuhusisha mtu wa kati (third party) kama benki au wakala. Inamaana unaweza kutuma kwenda mpokeaji bila kutegemea mabenki n.k.

Pia kila muamala unaofanyika unarekodiwa kwenye blockchain network. Hii inafanya wadukuzi kushindwa kudukua rekodi zako za miamala.

Hii inamaana blockchain inatunza rekodi za hela zako mithili Benki hufanya. Tofauti yake ni security na makato. Blockchain ina ulinzi mkali dhidi ya wadukuzi ukilinganisha na Benki. Pia makato ni madogo kwa blockchain.

BAADA KUONA HISTORIA FUPI TUANGALIE JINSI VIJANA WANAWEZA NUFAIKA.

Kama ilivyokawaida kwa biashara yoyote ile, uelewa ni kitu cha msingi sana kabla ya kuanza. Hivyo fursa hizi za kimtandao zinahitaji uelewa binafsi kabla ya kuanza kuwekeza.

Bila ya uelewa vijana wengi huwa tunapoteza hela zetu kwa sababu ya kukurupuka bila kulielewa soko. Mfano mzuri upo vijana wanaoikurupukia FOREX bila ya uelewa. Wakipoteza hela huita biashara hizi SCAM.

Kabla ya kuwekeza kwenye sarafu za kimtandao unatakiwa uelewe vitu vifuatavyo:

1. Unatakiwa uchague exchange wallet nzuri na halali. Wallet hizi zipo za aina mbili ambazo ni

(a). Centralized exchange wallet (yaani zipo chini ya regulations za serikali na zinajulikana kama kampuni). Mfano wake ni BINANCE, COINBASE, KRAKEN, REMITANO na LOCAL BITCOINS. Hizi zinahitaji kutambua mtumiaji (yaani Know Your Client).

(b). Decentralized exchange wallets ambazo zinaoperate kwenye blockchain network (ETHEREUM). Mfano mzuri ni Pancake swap n.k. Hizi hakuna haja ya kutambua mtumiaji.

Kwa watumiaji wapya centralized exchange wallets ni option nzuri. Binafsi natumia Binance na Kraken.

2. Unatakiwa kuelewa volatility ya sarafu unayonunua. Maana yake ni kuwa sarafu hizi hazina fixed price yaani bei elekezi. Hivyo kama ilivyokwenye hisa pendelea kununua ikiwa na bei ndogo (sio kwa zote). Mfano Bitcoin ilifika 60K USD mwezi April mwaka huu. Kama ulikurupuka ukanunua sasa hivi umepoteza nusu ya hela yako, (Ila kwa long-term investors hii haina effect kubwa kwani wao hutunza sarafu zao kwa miaka kadhaa).

3. Kama utatunza sarafu zako kwa long-term unatakiwa utumie cold wallets (zipo offline) ili kuepusha wadukuzi kuiba sarafu zako
 
Back
Top Bottom