Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 58,984
- 103,357
Chadomo mnakazi sana kifupi tulieni tutaelewana tu! Maandamano lini vile?
Ni sisi wapinzani wenyewe tutaweza kujitetea, kwa sasa ccm wamepoteza ushawishi kwa umma, hivyo wamejishika na vyombo vya dola ili kuendelea kututawala kwa shuruti. Namna pekee ni sisi wapinzani kugoma kushirikiana na wanaccm.Hii mtakoma tu! Hakuna rais anayeweza vumilia mtu kama Mbowe, anayejiita Mpinzani mkuu, lakini anashindwa kuchagua maneno ya kutumia majukwaani. Hii ni Afrika, hii ni TZ. Ukijifanya huogopi utaonyeshwa woga ulipo.
Watu walianza kumsifu Samia iwe kama rushwa kwake, ajikombe kwao. Sasa kibano kimekuja naona zinatungwa hadithi za kumtia woga.
Hakuna kushiriki msiba wala sherehe ama hafla yoyote ya mwanaccm, hakuna kununua chochote kwenye biashara ya mwanaccm, ama hata kupakia vyombo vyao vya usafiri labda iwe lazima sana. Tusiogope kuhamashana kwenye hili. Kwa vyovyote mbinu hii itamgusa kila mtanzania. Kwenye nyumba za ibada hakuna kutoa sadaka, na kuwaambia viongozi wa dini wanakalia kimya uovu. Mbinu hii haitatuacha na vilema wala kubambikiwa kesi, kutekwa ama kuuwawa. Mbinu hii ilitumiwa Zanzibar na ilifanya kazi.
Madai ya katiba mpya ni ya halali, kwanini wezi wa kura wasio na ushawishi waendelee kututesa na kutuumiza kwa madai yetu halali? Ni juu yetu wapinzani kujiokoa.