Je, Roma Mkatoliki anaandaliwa kuwa shahidi wa ICC?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,606
696,728
Nimeshangazwa na hadhi ya ukimbizi aliyopewa Roma Mkatoliki nchini Marekani. Hii pengine inatokana na kule kukamatwa kwake na wale WASIOJULIKANA kisha katika hali ya kushangaza sana na kwa muda uliopangwa Roma akapatikana akiwa hoi majeruhi na majeraha ya kuteswa.

Baada ya kupata nafuu majeraha yale ya mwili aliongea kilichompata. Lakini kukiwa na kila dalili kwamba alificha ama aliogopa kuongea mengi. Kutoka hapo Roma hakuwa sawa tena kama zamani. Kuna mzimu ulikuwa unamuandama.

Nusu ya pili ya mwaka jana 2019 Marekani na washirika wake wakaanza kutoa maangalizo na matamko kuhusiana na hali ya kuzorota kwa haki za binadamu, usalama na uhuru wa kutoa maoni. Ni katika kipindi hicho Roma alitimkia Marekani na hatimaye vikafuatia vikwazo kwa baadhi ya viongozi kusafiri na kuingia marekani sambamba na kunyimwa misaada na mikopo nk

Kwenye taarifa ya Marekani hawakumung'unya maneno walimtaja kiongozi mmoja kama wa kwanza kuwekewa kikwazo cha kusafiri Marekani.

Ni kiongozi huyo huyo aliyeahidi kupatikana kwa Roma ndani ya muda fulani naye pia akapatikana kweli. Kiongozi huyo ana lundo la tuhuma za kuteka. Waliotekwa na kupotea ni wengi. Ni Roma na wachache wamebahatika kutekwa na kurudi hai.

Kwenye taarifa ya Marekani wameweka wazi kuwa vikwazo ni hatua za mwanzo tu. Kwa maana hiyo hatua zaidi zinafuata. Je, ni hatua gani hizo? Je, ni mashtaka ICC?

Kama ni mashtaka ICC, Maana yake kutahitajika ushahidi usio acha shaka na mashahidi pia. Roma ni mhanga wa kutekwa na Marekani kaenda kama mkimbizi.

Huyu anaweza kuwa shahidi muhimu sana, hivyo kuepuka kudhurika ama kutishwa asitoe ushahidi pengine ndio maana kakimbiziwa mbali aje kumkaanga mtu. Wengine ni Msaidizi wa Membe na Msaidizi wa Zitto wako wapi hawa?

Jr™️
 
CCM wajipange, mabeberu safari hii wataondoka na vichwa vingi sana utawala huu.

Kidogo kidogo wameanza kula "MATAPISHI" yao, wamepeleka muswada bungeni (kama kawaida yao kwa HATI YA DHARURA) kuomba sheria ya Arbitration ibadilishwe ili migogoro ya madini iwe inasuluhishwa kwenye Mahakama Ya Biashara Ya Kimataifa.

Kwa mtazamo wangu, watu wasiojulikana watakuja kufanya "MAAMUZI" magumu sana kwa yule "MKUU WA MIKOA YOTE TANZANIA", ili kuficha aibu yao.

Principal Ya Dunia "STAGE 1: Unatumiwa mpaka umuhimu wako utakapokwisha, ukiisha umuhimu wako inafuata STAGE 2: Disposition (Wanaku dispose)"

To be continued. . . . . . .
 
72 Reactions
Reply
Back
Top Bottom