Je Rasimu hii ya Katiba ni nchi gani?

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,417
3,154
Nimeisoma Rasimu ya Katiba, nimepata simtofahamu juu ya hasa Rasimu hii ni ya nchi gani.
Nasema hivyo kwa kuwa, Rasimu inayaongeleea mambo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku ikisema ya kwamba, masuala ya Washirika wa Muungao (Tanzania Bara na Zanzibar), yasiyo ya Muungano yataamuliwa na Katiba za Washirika wa Muungano.
Utata unakuja pale ambapo wote tunajua ya kwamba Tanzania Bara haina Katiba yake, ila Zanzibara wanayo.

Maswali ya kujiuliza:
A. Je masuala yasiyo ya Muungano yataamuliwa na Katiba ipi?
B. Je Zanzibar waliyajua haya hata wakatengeneza Katiba yao?
C. Ikiwa kama Rasimu hii itapita na kuwa Katiba, je uchaguzi wa 2015, muundo wa serikali n.k vitaamuliwa na Katiba ipi?

Naomba wenye uelewa wanifafanulie. Ikiwa kama Katiba ya Tanzania (ya sasa) ndiyo itakayobatizwa na kuwa Katiba ya Tanzania Bara, pia ningependa kujua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom