Je, Rais yupo humu? Kama yupo ina maana hatuoni?

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Si kwa ubaya hivi mama yupo humu ndani? Nawaza kwa sauti na kama yupo kwa mikeka yake hatuoni humu ndani?

Humu wapo Watu wameanza kuunga mkono juhudi zake licha ya kuunga kwani hawaoni/Hatuoni? Wapo wengine kipindi kile walipishana na Mheshimiwa Rais wa kipindi kile na sasa wanamsifu na kuungana na Mheshimiwa Rais wa sasa.

Kweli Mama humuoni Pascal Mayalla kama si yeye yupo USSR japo sifahamu kuwa ni nani huenda yeye akawa hata ndio mchengerwa mwenyewe inamaana na hata Shimba Ya Buyenze maana siku hizi na yeye amekukubali.

Hitimisho na hata mimi kweli?
 
Hivi kwa nini huyu mama hapendwi sana mtaani, kila mmoja anamponda unless watumishi serikalini na baadhi ya wanufaika.

Lakini kiukweli raia mtaani wachache sana wanamzungumzia vyema.
Yuko bize kutafuta uungwaji wa wazee wakongwe wa chama 2025, kwa kuwapatia watoto wao mavyeo serikalini huku anademka kwa kutwambia tuzione fursa tuzichangamkie.
 
Bila shaka alieandika uzi huu na wanaoandika comment wote ni mtu mmoja alieamua kuwa na ID tofauti ili kuvuna data nyingi kutoka kwa yule katibu mkuu wa chama matata cha upinzani. Haya endeleeni kujitekenya na kucheka wenyew.
 
Ana matumizi mabaya na ofisi kwa kugawa vyeo kwa maswahiba ili ajiimarishe kisiasa.
CHADEMA nao wasingekua disorganized wangechukua nchi 2025 ila ukiwatizama yaani bora hata CCM iendelee kutawala tu. Dah nchi yangu Tanzania, hakika umepata mkosi
Hivi mkuu ungekua mwenyekiti wa Chadema kwa hali iliopo na iliyopita ungefanya Nini???kwa makatazo yote hayo wewe ungefanyaje!!??vaa viatu vya Mbowe halafu unambie!!
 
Hivi kwa nini huyu mama hapendwi sana mtaani, kila mmoja anamponda unless watumishi serikalini na baadhi ya wanufaika.

Lakini kiukweli raia mtaani wachache sana wanamzungumzia vyema.
Wasiompenda shauri zao. Sisi watumishi ndo mainjinia wenyewe, tukimkubali Sisi ujue kashashinda huyo 2025.
Mama wanaokupenda hawakwambii, na wanaokuchukia hawakujui....upo moyoni.
 
Mmmmmmhh mbona umeharibu kwa kutumia wingi ? Sema wewe ukimkubali amepita , mimi ni mtumishi wa serikali yake lakini simkubali na watumishi wenzangu tukikaa huwa tunaponda sana mama huyu , hatufai hata kidogo , natamani kusikia nchi imemshinda .
 
L
Mmmmmmhh mbona umeharibu kqa kutumia wingi ? Sema wewe ukimkubali amepita , mimi ni mtumishi wa serikali yake lakini simkubali na watumishi wenzangu tukikaa huwa tunaponda sana mama huyu , hatufai hata kidogo , natamani kusikia nchi imemshinda .
Labda utakuwa mtumishi wa ndani halafu una certificate😂 mnakuaga na roho mbaya zisizo na sababu😂...Sisi tuliopandishwa madaraja mwaka Jana na kuondolewa retention fee kwenye mkopo wa bodi hutuambii kitu....kaa na wenye degree waulize.
 
Ana matumizi mabaya na ofisi kwa kugawa vyeo kwa maswahiba ili ajiimarishe kisiasa.
CHADEMA nao wasingekua disorganized wangechukua nchi 2025 ila ukiwatizama yaani bora hata CCM iendelee kutawala tu. Dah nchi yangu Tanzania, hakika umepata mkosi
Hao chadema wenyewe Viti maalum wanawapa wake zao na vipenzi vyao refer kina Mukya, Hawa Bananga...basi Tu hawajapewa nchi tungeyaona maajabu kwenye teuzi zao pia.
Huwezi kufanya Kazi na watu usiowajua vizuri, Yani uokote mtu huko umpe uwaziri, awe ndo msaidizi wako...hata wewe tukikupa nchi huwezi kufanya hivyo....muhimu nchi isonge, tunachohitaji Sisi ni maendeleo.
 
Hivi kwa nini huyu mama hapendwi sana mtaani, kila mmoja anamponda unless watumishi serikalini na baadhi ya wanufaika.

Lakini kiukweli raia mtaani wachache sana wanamzungumzia vyema.
Maisha yao yamekua magumu sana uhakika wa kifedha na vitu kupanda bei bila pesa kuongezeka.
Biashara huku chini ni ngumu sana mauzo yameshuka kwa kiwango kikubwa sana na hasa tozo zilipoingizwa zikagongelea msumali.
 
L

Labda utakuwa mtumishi wa ndani halafu una certificate mnakuaga na roho mbaya zisizo na sababu...Sisi tuliopandishwa madaraja mwaka Jana na kuondolewa retention fee kwenye mkopo wa bodi hutuambii kitu....kaa na wenye degree waulize.
Hiyo neema ya promotion imekugusa wewe mchumia tumbo lako na uzao wako .
 
Mmmmmmhh mbona umeharibu kqa kutumia wingi ? Sema wewe ukimkubali amepita , mimi ni mtumishi wa serikali yake lakini simkubali na watumishi wenzangu tukikaa huwa tunaponda sana mama huyu , hatufai hata kidogo , natamani kusikia nchi imemshinda .
Uchukie au umpende hakuna kitu utakachobadilisha.

Wasimamizi wa uchaguzi ni DEDs na WEO/VEO ambao wote ni watiifu wa Samia.

Hata akitaka kushinda kwa 100% atashinda tu na hakuna kitu chochote utafanya.
 
Haya ni mawazo yako , ogopa anayepingwa sana , sina uhakika hata uliowataja kama wanamuunga mkono mama, sana sana wanamnanga tu.
 
Zinduka uuone UHALISIA.

Achana na hisia na fantasy ambazo ni kama haziwezekani.
 
Mmmmmmhh mbona umeharibu kwa kutumia wingi ? Sema wewe ukimkubali amepita , mimi ni mtumishi wa serikali yake lakini simkubali na watumishi wenzangu tukikaa huwa tunaponda sana mama huyu , hatufai hata kidogo , natamani kusikia nchi imemshinda .
Iwe toinamagezi kalyee mpali. Mimi nimtumishi namkubali Sana tuu. Huyo shetani wenu amebinya haki zetu miaka mitano huku akitutolea maneno ya shombo na hao waliobatizwa jina la unyonge wakitucheka nakuweka midimo juu Kama beberu kwa furaha ya mateso yetu. Sasa kaja mama muungwana , mstaraabu watu wamelipwa malimbikizo yao, wamepandishwa madaraja, na bado mwaka huu atapandisha mishahara. Lakini katupunguzia madeni bodi ya mikopo kwa kuondoa makato ya kikatili yaliyo wekwa na huyo shetani wenu. Wastaafu sasa hivi wanalipwa kwa wakati. Sasa mtu kamu huyu utaanzaje kumchukia? Mimi kila siku namuombea kwa Mungu ampe afya njema tu . Nakila ninapokuta wanamuongelea vibaya najenga hoja za kumtetea nawatu wanaelewa maana watanzania wengi nifuata mkumbo hawelewi Mambo mengi.
 
Si kwa ubaya hivi mama yupo humu ndani? Nawaza kwa sauti na kama yupo kwa mikeka yake hatuoni humu ndani?

Humu wapo Watu wameanza kuunga mkono juhudi zake licha ya kuunga kwani hawaoni/Hatuoni? Wapo wengine kipindi kile walipishana na Mheshimiwa Rais wa kipindi kile na sasa wanamsifu na kuungana na Mheshimiwa Rais wa sasa.

Kweli Mama humuoni Pascal Mayalla kama si yeye yupo USSR japo sifahamu kuwa ni nani huenda yeye akawa hata ndio mchengerwa mwenyewe inamaana na hata Shimba Ya Buyenze maana siku hizi na yeye amekukubali.

Hitimisho na hata mimi kweli?
Jf connection yake haitoshi kupata fulsa,

Kaa karibu na familia kubwa kubwa,mfano Msoga n.k hutochukua week , utakua umeula
 
Back
Top Bottom