Je, Rais Samia na PM wameamua kutumia usafiri wa umma ku-cut cost kwenye ziara zao? | Majaliwa alitua Kigoma kwa Precision, Rais akaondoka na Emirates

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,542
2,172
Nawasalimu kwa Jina la JMT,

Katika kile kinachoonekana kuishi na kufanya|kutenda Kizalendo kwa Rais na Waziri Mkuu wetu Mhe Majaliwa Khasim Majaliwa pamoja na kwamba Tanzania tunajumla ya ndege mpya 11 wao wameamua kwenye baadhi ya shughuli zao za kiserikali zinazotumia gharama kubwa ya ndege na maeneo hayo kama kunandege watatumia usafiri huo wa Umma,

Tarehe 16|09|2021 waziri mkuu alipanda " Precision Air line " kwenda Kigoma kwenye ziara ya kikazi wakati tarehe 19|09|2021 Rais Samia alipanda Emirates Air line kwenda New York Marekani kwaajili ya kuhudhuria mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,

Sote tunafahamu,Umbali kutoka Kigoma -Dar es salaam ni km 1,081 sawa na masaa 2:30 angani,Hii kwahakika ni Safari ndefu na inatumia gharama kubwa za Serikali ndio sababu Waziri mkuu aliamua kutumia Usafiri wa Umma yaani Precision Air Line ambayo inafanya Safari zake Kigoma- Dar kwa zaidi ya miaka 15 Sasa,

Watanzani ondoeni shaka nchi yenu iko Salama sana pengine tangu kuumbwa kwake,


VIVA MAJALIWA VIVA ||VIVA SANIA VIVA

 
Kelele zetu zjmelipa,maana kuna kipindi Samia alikuwa na Airbus na Makamu akawa na Airbus huku PM akiwa na Bomberdier!
Swali:Hiyo ndege imekodiwa au amesafiri kama abiria?
 
Wapinzani wetu walimsifia Rais wa jirani kwa kupanda usafiri wa umma, na kumzodoa huyu wetu kuwa ameenda na dreamliner, bila hata ya kuwa na uhakika!! Walipogundua wameingia chaka kwenye hilo, wakaanza kumzodoa kwa mambo mengine ya hovyo na ya kitoto kabisa!! Wengine wakasema amekodi ule mdege wa Emirates wote! Kudeal na Opposition wa TZ yataka moyo sana
 
Najivunia kuwa raia wa TANZANIA.

Najivunia kuwa na rais wetu kipenzi chifu mkuu Mh. Hangaya SSH!

Najivunia kuwa na makamu wa Rais Mh. Philip I.Mpango na PM Mh. Kassim Majaliwa 💪👍👊😍

#NchiKwanza
#SiempreJMT
 
Hiyo kwenye video iliyoambatanishwa ni Precisionair?

Tufanye ni yenyewe, kwamba ilikua na abiria wengine akashuka kwanza yeye kwenye zulia jekundu na abiria wakaenda kushushwa eneo la abiria ama ilikuaje? Nauliza tu nifahamishwe!
 
Wapinzani wetu walimsifia Rais wa jirani kwa kupanda usafiri wa umma, na kumzodoa huyu wetu kuwa ameenda na dreamliner, bila hata ya kuwa na uhakika!! Walipogundua wameingia chaka kwenye hilo, wakaanza kumzodoa kwa mambo mengine ya hovyo na ya kitoto kabisa!! Wengine wakasema amekodi ule mdege wa Emirates wote!! Kudeal na Opposition wa TZ yataka moyo sana
Tanzania haina wapinzani "credible"....
 
Wanasafiri na watu wa kawaida au wanakodi? kama wanakodi nini utofauti kati ya kutumia ndege za serikali na kuzilipia na kutumia za binafsi na kulipia?

Watanzania wanapenda kuona serikali inapunguza gharama zisizo za msingi kwani ni kodi za wananchi hizo. Kutumia ndege za kukodi haliwezi kuwa jibu la kuondokana na matumizi makubwa na ysiyo ya msingi.

Wananchi lazima watahoji kuhusu gharama za ndege za kukoadi maana isije ikawa mwanya mwingine wa upigaji
 
Hiyo kwenye video iliyoambatanishwa ni Precisionair?

Tufanye ni yenyewe, kwamba ilikua na abiria wengine akashuka kwanza yeye kwenye zulia jekundu na abiria wakaenda kushushwa eneo la abiria ama ilikuaje? Nauliza tu nifahamishwe!
Wewe unadhani haiwezekani?

Acheni Roho mbaya Serikali inafanya kazi kubwa sana hii
 
Wanasafiri na watu wa kawaida au wanakodi? kama wanakodi nini utofauti kati ya kutumia ndege za serikali na kuzilipia na kutumia za binafsi na kulipia?
Watanzania wanapenda kuona serikali inapunguza gharama zisizo za msingi kwani ni kodi za wananchi hizo.... kutumia ndege za kukodi haliwezi kuwa jibu la kuondokana na matumizi makubwa na ysiyo ya msingi.
Wananchi lazima watahoji kuhusu gharama za ndege za kukoadi maana isije ikawa mwanya mwingine wa upigaji,,,,,,,,,
Hujawahi kupanda ndege kabisa we mtu,

Mbona haya mambo ya kawaida sana tu,

Ndio maana ya Uzalendo hii
 
Back
Top Bottom