Eti hoja mufilisi... hoja mufilisi au HUELEWI!!Hoja yako ni mufilisi.
Kwahiyo kama angekuwa amegombea, ndo angeweza kuongoza mambo ya bara yasiyo ya muungano?!Huwezi kutenganisha Urais alioupata Samia bila kuweka Uzanzibari wake.
REMEMBER, kama angegombea usingeangaliwa u-ZNZ wake bali Utanzania wake!!
Na kwa mawazo yako, kwavile hakugombea basi mamlaka yake yanakuwa tofauti kulinganisha kama angegombea wakati anatumia katiba ile ile na sheria zile zile?! Kwamba, kwavile ametokea kuwa VP, basi urais wake hauwezi kuwa kama yule ambae aligombea?!
Sio kutenganisha... niliweka wazi mapema kwa sababu nilishashuku kwamba huenda unau-judge urais wake sio kama rais bali kama rais aliyekuja kuwa rais akitokea kuwa VP!Katiba imetamka, Rais akifariki, Makamu( ambaye ni lazima atoke Zanzibar) anarithi kiti. Sasa unatenganishaje haya mawili.
Unashindwa kufahamu kwamba, a moment alipoapishwa, huyu akawa rais na u-VP wake ukakoma hapo!
Na kwavile akaja kuwa rais, ana wajibu na mamlaka ya kuhudumu kama rais bila kuangalia kama alisimama majukwaani kuomba achaguliwe kuwa rais, au vinginevyo!
Muhimu ni kwamba, urais wake ni halali kwa mujibu wa katiba!
Na nimeshakuambia, sifa ya mtu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kwa mhusika kuwa raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano, PERIOD!Lakini hoja yangu sio Samia kuwa Rais wa JMT. Hoja yangu ni Samia kuongoza mambo ambayo siyo ya muungano as per constitution. Over!!!!!
Na hakuna popote kwenye katiba panaposema rais aliyechaguliwa majukumu yake ni haya, na yule ambae ameingia akitokea kuwa VP, majukumu yake ni haya!
Na hakuna inaposema Rais wa Jamhuri anayetokea ZNZ majukumu yake ni haya na yule anayetokea bara, majukumu yake ni haya!
Na katiba haijasema kwa sababu hicho kingekuwa ni kiroja!!