Je, Rais Samia anayo haki na misingi ya kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) kwa mambo yasiyo ya Muungano?

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
526
583
A. UTANGULIZI
Napenda kuweka wazi kwamba nimeanzisha mjadala huu, ili kuondoa mkanganyiko na mkwamo ninao uona wazi wazi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania. Kwa mara nyingine katiba yetu imejaribiwa (imekuwa tested), hivyo ni busara kuwepo kwa mjadala wa kuondoa shaka na hoja gonganishi katika katiba yetu kwa ustawi bora na imara wa Taifa letu Pendwa.

B. HISTORIA KIDOGO
Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania iliundwa Tar.26 April 1964, ikiwa ni muungano wa maTaifa huru ya Jamhuri ya Tanganyika (1962) na Jamhuri ya watu wa Zanzibar (1964). Jamhuri hizi mbili ziliingia mkataba wa pamoja 1964 na kuanzisha dola la Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Katiba ya J.M.T ya mwaka 1977, ibara ya 4(3) imeorodhesha mambo 22 ya muungano baina ya pande mbili zilizo-ungana.
Kwa upande wa Tanzania bara (Tanganyika) mambo yasiyo ya muungano yanasimamiwa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, na Kwa upande wa Zanzibar, mambo yasiyo ya muungano yanasimamiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Kwa Lugha rahisi, Muungano wetu ni wa serikali Mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika ilifutwa na haipo.

C. MAMBO YA MUUNGANO
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), ibara ya 4, ibara ndogo ya 3, imetoa mwongozo kuhusu mambo ya muungano. Na, yameorodheshwa katika nyongeza ya kwanza ya katiba yetu.
Yafuatayo ni mambo 22 ya muungano kwa mujibu wa Katiba yetu.
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.
9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
10.Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni.
13.Leseni ya viwanda na takwimu.
14.Elimu ya juu.
15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na gesi asilia.
16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
17.Usafiri na usafirishaji wa anga.
18.Utafiti.
19.Utafiti wa hali ya hewa.
20.Takwimu.
21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine yanayohusiana navyo.

Angalau kwa mujibu wa katiba yetu, haya yaliyo orodheshwa ndiyo mambo ya muungano.


D. HOJA MEZANI (HOJA KINZANI)

Kwa kuwa Rais aliyeko madarakani ni asili ya Zanzibar, hivyo ni mZanzibari, na anaongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na yeye ni zao la muungano wetu. Na, kwa kuwa Katiba yetu imebainisha dhahiri mambo ya muungano, Je? Ni sahihi kwa Rais wa sasa kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) hata kwa mambo yasiyo ya muungano?

1.Kama ni sahihi, anaongozaje mambo yasiyo ya muungano ilhali yeye ni mZanzibari na ni zao la muungano na ana uishi muungano pamoja na mambo ya muungano, tukumbuke kwamba , tumeungana lakini hatujaungana katika mambo yoye, tumechagua mambo ya kuungana.
2.Kama sio sahihi nini kifanyike?

E. HITIMISHO
Kuna watu mtaacha kujibu hoja na kuleta vioja, kuna watu mtauliza kwa nini hoja hii inaletwa sasa. Majibu yake ni kwamba, Jana(26.04.2021) ilikua siku ya kukumbuka Muungano wetu, hivyo ni busara kuujadili kipindi hiki, na jana kuna kongamano lilifunguliwa ,kuendeshwa na makamu wa Rais Dkt.P.Mpango. Lakini, kwa maya nyingine tumepata Rais Mzanzibar kwa mujibu wa Katiba, hivyo nimeona ni vyema tujadili jambo hili ili kutoa/kuondoa hoja hizi kinzani.

Kwa maoni yangu, Kuna haja ya kuangalia maslahi ya Tanzania bara(Tanganyika) katika muungano wetu. Sioni maana ya Mzanzibari kuwaongoza waTanganyika katika mambo yasiyo ya muungano, unless tukubali kuungana kwa kila jambo. Pia, kuna haja ya kuwalinda waTanganyika kama ambavyo katiba inawalinda waZanzibari, Mathalani;
-Mtanganyika hawezi kumiliki ardhi Zanzibar kwa hoja mufilisi kwamba Zanzibar ni ndogo, lakini kwenye mgawanyo wa pesa za Maadhimisho ya Muungano watataka equal share.
-Wakati anahutubia Bunge, Rais Samia alitoa ahadi ya kununua Meli za uvuvi nne, huku mbili zikielekezwa Zanzibar na mbili Bara. Kwanza hii sio haki, kwani Uvuvi, na Usafirishaji wa majini siyo mambo ya muungano, sioni matiki kwa nini Rais wa Muungano aanze kuhangaika na mambo yasiyo ya muungano kwa Zanzibar kwa kutumia pesa za Watanganyika.

Niko Tayari kurekebishwa na kusahihishwa katika mjadala huu, ili tujenge Muungano utakao kidhi matakwa ya pande zote za Muungano.
 
Yaan mzanzibari aongoze bara kwa mambo hata yasiyo ya muungano ila Mbara asiingilie mambo yasiyo ya muungano Zanzibari! asee Nyerere alikosa hekima katika hili.
Bora hata wangejitawala wenyewe. Kama wangeamua kutawalia na Sultan wao wa Oman, wangejua wenyewe. Huu Muungano hauna tija wala faida yoyote ile kwa Tanganyika!

Kama hofu ilikuwa ni Vita Baridi, kwa sasa havipo tena! Kwma vipi wakabidhiwe tu Visiwa vyao, na sisi tuendelee na nchi yetu.
 
Tuelewe kwamba Zanzibar ilipata Uhuru wake kutoka kwa Waingereza 1963 lakini wazalendo walitaka kumuondoa Sultan na walifanikiwa kufanya hivyo mwaka1964.

Sultan alikimbilia Uingereza lakini nchi yake ya asili yaani Oman ilikua tayari kumpa msaada wa kijeshi arudi Zanzibar. Wazalendo waliomba msaada Bara na huu muungano kuzaliwa.
 
Tuelewe kwamba Zanzibar ilipata Uhuru wake kutoka kwa Waingereza 1963 lakini wazalendo walitaka kumuondoa Sultan na walifanikiwa kufanya hivyo mwaka1964.

Sultan alikimbilia Uingereza lakini nchi yake ya asili yaani Oman ilikua tayari kumpa msaada wa kijeshi arudi Zanzibar. Wazalendo waliomba msaada Bara na huu muungano kuzaliwa.

Wazalendo ni wakina nani?
Labda nikuulize, Mwalimu Nyerere alishauriana na nani? Kabla hajatuunganisha na Zanzibar?
 
Je wewe ni Mtanganyika?Unataka kuwa Mtanganyika?Unautaka Utanganyika?Je unafikiri kwamba Rais wa Muungano kuwa Mzanzibari ni Kosa?Je unafikiri ni tatizo la Kikatiba?Unaumia maendeleo kuwepo Zanzibar?Unataka Tuvunje Muungano?Unataka tumnyanganye Samia Urais kwa sababu yeye ni Mzanzibar?Unafikri kwamba kuwa mzanzibari kuna mfanya asiwe na maslahi na Tanganyika?

Je unafikiri katia ya Tanganyika na Zanzibar nani anauhitaji Muungano?Unafikiri ni kwa nini Zanzibar ina Rais wao na Katiba yao?SItaki kuweka majibu ya maswali haya hapa ila nakubaliana na wewe kwamba Katiba yetu iko katika majaribu mazito sana.Swali ni Je.Tuirudishe Tanganyika?Tuiondoe Zanzibar?Kuwe na Mfumo wa Makamu wawili wa Rais.Ambapo Makamu wa kwanza ni Mtanganyika na Wa pili ni Mzenjibara?

Sijui unachotaka ni nini ila nafikiri kwa sasa tuache chokochoko tuache kazi iendelee.Tusipande mbegu ya ubagudhi ila tujadili kwa haki na uwazi
 
Nadhani tukubali kuwa Magu hayupo tena, tumkubali Samia na maisha yatakua rahisi tu. Sisi ndio tuliibiwa kura na hao akina Samia lakini tumekubali yaishe, mbona nyie CCM hamtaki?

Nadhani ungejibu hoja sio vioja, baki kwenye mada
 
Nadhani tukubali kuwa Magu hayupo tena, tumkubali Samia na maisha yatakua rahisi tu. Sisi ndio tuliibiwa kura na hao akina Samia lakini tumekubali yaishe, mbona nyie CCM hamtaki?
Umeongea point Mkuu. Tatizo hapa sio Uzanzibari, si umwanamke wala sio Muungano. Tatizo ni kutotaka kukubaliana na ukweli kuwa Magufuli hayupo tena na haitokaa kamwe arudi. Kummithilisha Samia na Magufuli ni kutomtendea haki Samia. Katiba ndio imemuweka hapo alipo hivyo kwa sasa tukubaliane tu na hilo maisha yasonge.
 
Nakushairi uachane na kutaka kujua mimi ni nani, acha kunijadili mimi na jadili hoja.

Mbona jambo ni rahisi sana, tumeungana katika mambo 22, kwa upande wa Zanzibar wana chombo kinacho deal na mambo yasiyo na muungano, kwa upande wa Bara hakuna chombo kama cha Zanzibar pindi rais wa Jamhuri anapotoka Zanzibar.

Tujadiliane kwa hoja na kwa kujenga sio kuitana majina
 
Zanzibar ni nchi kamili ndio maana kwao kuna mambo yasiyo ya Muungano.

Sasa wewe bwashee nchi yako ni ipi hadi useme una " vitu" visivyo vya muungano?!

Kwa hiyo hayo mambo yasiyo na muungano yako upande mmoja tu?

Soma Katiba my friend, mambo yasiyo ya muungano ni kwa pande zote mbili.

Iweje Mzanzibari aongoze Bara kwa mambo yasiyo ya Muungano?
 
Nakushairi uachane na kutaka kujua mimi ni nani, acha kunijadili mimi na jadili hoja.

Mbona jambo ni rahisi sana, tumeungana katika mambo 22, kwa upande wa Zanzibar wana chombo kinacho deal na mambo yasiyo na muungano, kwa upande wa Bara hakuna chombo kama cha Zanzibar pindi rais wa Jamhuri anapotoka Zanzibar.

Tujadiliane kwa hoja na kwa kujenga sio kuitana majina
Chombo Kipo ni Waziri Mkuu,Mamlaka yake ni ya BARA peke yake.Unataka Waziri Mkuu awe na madaraka sawa na ya Rais wa Zanzibar?
 
Muundo wa muungano uliopo ni kaburi kwa Tanganyika
(Umeifanya Tanganyika kuwa ya kunyonywa na kutawaliwa na Zanzibar)
  • Zanzibar haichangii gharama za uwekezaji na uendeshaji ila mgao wa mapato, faida, bakaa inapata
  • Kule Zanzibar hakuna mtanganyika anayeruhusiwa kumiliki ardhi ila bara wazanzibari wanajitwalia tuu
  • Kule Zanzibar hakuna mtanganyika anayeruhusiwa kuajiliwa SMZ lakini wazanzibari wanaajiliwa mpaka ualimu na ajira za kada ya afya
  • Kule Zanzibar hakuna mtanganyika anayeruhusiwa kugombea uwakilishi ila bara wanagombea tuu
  • Kule Zanzibar hakuna mtanganyika anaeteuliwa kushika nafasi za uongozi kwenye serikali ya Zanzibar ila bara wanateuliwa kuwa ma DAS, DED, DC, RAS, nakadhalika
 
Umeongea point Mkuu. Tatizo hapa sio Uzanzibari, si umwanamke wala sio Muungano. Tatizo ni kutotaka kukubaliana na ukweli kuwa Magufuli hayupo tena na haitokaa kamwe arudi. Kummithilisha Samia na Magufuli ni kutomtendea haki Samia. Katiba ndio imemuweka hapo alipo hivyo kwa sasa tukubaliane tu na hilo maisha yasonge.

Kama mngrjikita kujibu hoja basi tungefika mbali sana. Je, nimeandika uongo? Au kuna sehemu nimekosea?
Magufuli kaingiaje hapa?

Hoja ni hii, ni sahihi kwa Mzanzibar kuongoza Bara kwa mambo yasiyo ya Muungano??
Tubaki hapa jamani
 
Back
Top Bottom